Miongoni mwa miradi ya Maahadi ya Qur’an tukufu: ni mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’an katika swala…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu inatekeleza miradi mingi ya Qur’an tena ya aina mbalimbali, miradi yote inalengo moja kuu, nalo ni kuingiza utamaduni wa kushikamana na Qur’an tukufu kwa watu wa tabaka zote, wanatumia fursa zote na muda mzuri wa kufikia lengo hilo, miongoni mwa miradi hiyo, ni mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’an katika swala, ambao hutekelezwa kipindi cha ziara ya Arubainiyya, Muharram na ziara ya Shaabaniyya katika barabara zinazo elekea kwenye malalo matukufu ya Karbala, na katika siku za kawaida mradi huo hutumia uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kuendeshea darsa zake, huwafundisha mazuwaru usomaji sahihi wa sura za Qur’an ambazo husomwa mara nyingi katika swala.

Mradi huu umezingatia kua swala ndio nguzo kuu ya dini, ikikubaliwa na vingine vitakubaliwa na ikikataliwa na vingine vitakataliwa, kwa hiyo tumejikita katika kufundisha usomaji sahihi wa sura zinazo somwa mara nyingi katika swala za faradhi za za sunna, miongoni mwa sura hizo ni, surat Fat-ha, Ikhlasi na Kauthar, tuligundua kua kuna idadi kadhaa ya mazuwaru hawajui kusoma sura hizo au wanazisoma kimakosa, jambo linalo tia wasiwasi kuhusu utekelezaji wao wa nguzo ya swala, pia wanafundishwa na nyeradi za swala ambazo ni muhimu katika kukamilika swala.

Jambo hili linafanywa na wasomi wa Maahadi, mazuwaru wanafundishwa kwa kutumia folda (pakeji) inayo ainisha maeneo yote ambayo hukosewa mara nyingi katika usomaji, upande wa haraka au matamshi ya herufi, zairu huambiwa asome kisomo cha swala, kwa hiyo husoma kama anavyo soma katika swala kisha hurekebishwa sehemu atakazo kosea na kufundishwa matamshi sahihi.

Mradi huu unamwitikio mkubwa sana kutoka kwa mazuwaru, kwa sababu njia ya ufundishaji ni nzuri na hutolewa mifano hai inayo msaidia msomaji kutofanya makossa katika siku zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: