Nafasi ya Abulfadhil Abbasi kwa mama yake Ummul Banina (a.s)…

Maoni katika picha
Pamoja na kwamba mama huwa na mapenzi kwa mwanaye ya umama, yanayo tokana na kubeba mimba, kumnyonyesha na kumlea mtoto, lakini mapenzi ya Ummul Banina (a.s) kwa mwanaye Abbasi yalikua zaidi ya mapenzi ya umama, alikua na mapenzi makubwa zaidi, kutokana na kutambua utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ukubwa wa imani yake pamoja na mapenzi aliyo kuwa nayo kwa ndugu yake na Imamu wake Hussein (a.s).

Pamoja na ikhlasi kubwa aliyo kuwa nayo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake nadini yake na Imamu wake, sambamba na sifa nzuri alizo kuwa nazo na tabia njema; Abulfadhil Abbasi (a.s) alikua na kila aina ya uzuri, ulio anza kuonekana tangu wakati wa kuzaliwa kwake bali kabla hata ya kuzaliwa, mama yake Ummul Banina alimpa nafasi kubwa mno, ndipo tunamkuta mama yake akimlinda na mabaya wakati wa utoto wake anasema:

Namlinda kwa utukufu wa Mmoja… kutokana na kila jicho la hasidi.

Aliye simama na aliye kaa … mwislamu na asiye kua mwislamu.

Mpitaji na mkaaji … aliye zaliwa na mzazi.

Kuna maneno mengine aliyo sema:

Ewe ambaye umemuona Abbasi kua burudisho … mbele ya halaiki ya watu.

Ni miongoni mwa watoto wa Haidari … walio kua na ushujaa mkubwa.

Niliambiwa kuwa mwanangu ameuawa … kapigwa kichwani kwake na kukatwa mikono.

Hakika alikua simba mwenye juhudi … akapigwa na chuma kizito kichwani kwake.

Kama panga lako lingekua mkononi mwako … asinge kusogelea yeyote.

Na maneno yake mengine anasema:

Msiniache mkiwa Ummul Banina … mnikumbuke kwa simba nilizo kuwa nazo.

Nilikua na watoto wa kuwaita … leo nimekua sina watoto.

Watoto wote wanne … wameuawa kwa kukatwa vichwa.

Walivamiwa na watu waovu … wakauawa wote kwa pamoja.

Kama ningeambiwa mapema … kuwa Abbasi amekatwa kichwa.

Ndio, Hakika Ummul Banina (a.s) alikua mtu wa kwanza kumuhimiza Abbasi (a.s) apigane kwa ajili ya kuwahami bani Twalib, alikua anakwenda katika makaburi ya Baqii analia na kuwahusia watoto wake wanne –Abbasi (a.s) na ndugu zake Abdullahi, Jafari na Othmani- akiwapa usia mkali, watu walikua wanakusanyika kumsikiliza namna anavyo lia na kuhusia halafu na wao wanalia pamoja naye, hata Marwani aliyekua adui mkubwa wa bani Hashim alikua anapo pita Baqii akisikia sauti ya Ummul Banina, anasogea na anakaa na kuanza kulia pamoja na watu wengine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: