Marjaa dini mkuu ataja mambo muhimu yanayo pelekea kufanikiwa utowaji wa huduma za umma…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu ametaja mambo muhimu yanayo pelekea kufanikiwa utowaji wa huduma za umma, ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) Ijumaa ya leo (6 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (20 Julai 2018m), chini ya uimamu wa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, mambo hayo ni:

Jambo la kwanza: Mtu anaye taka kuto huduma lazima awe anaijua huduma anayo taka kuitoa, hili ni jambo la kawaida, haiwezekani mtu mmoja akatoa huduma za aina zote, lazima niifahamu huduma ninayo taka kutoa, siwezi kuahidi kutoa huduma ya matibabu wakati sijui tiba, wala siwezi kuahidi kutoa huduma kwa watu ambao sijui wanataka huduma gani, lazima nijuwe ninacho taka kufanya, ili nitakapo kifanya nikifanye kwa ustadi kutokana na ujuzi wangu katika jambo hilo.

Jambo la pili: Unapo taka kutoa huduma lazima uwe na vifaa vizuri vitakavyo kuwezesha kutoa huduma bora, kwa mfano unapo taka kutoa huduma ya matibabu lazima uwe na vifaa vizuri na upate wasaidizi watakao kuwezesha kufanya kazi yako kwa ufanisi, kila huduma inayo hitajika inavyo kua kubwa ndivyo unavyo hitajia vifaa vizuri na wasaidizi imara zaidi.

Jambo la tatu: Ninapo taka kutoa huduma lazima nijuwe muda wa kutoa huduma hiyo, haiwezekani kusema tu nitatoa huduma na muda upo, lazima nibainishe muda halafu nijipime naweza au siwezi, kuchunga muda ni muhimu sana, na kuharakisha kutoa huduma ni bora zaidi, kwa mfano wewe unataka kuniokoa kisimani nenda haraka katafute kamba uje uniokoe, unatakiwa utowe huduma hadi ikamilike ndani ya muda muwafaka.

Jambo la nne: Nalo ni muhimu zaidi.. lazima kuwepo na kuaminiana baina ya mtowa huduma na mpewa huduma, lazima kila mmoja amuamini mwenzake, ili waweze kusaidiana, kwa mfano mbele yangu kuna wagonjwa kumi na wote natakiwa niwape huduma ya matibabu, lazima waniamini na mimi niwaamini, huduma inatakiwa itolewe lakini lazima kuwe na kuaminiana kati ya pande mbili, kuaminiana huko ndiko kutakako fanya kazi ifanyike vizuri, huduma sio jambo la nadhariya bali ni vitendo halisi, mimi kama ni mgonjwa, nisema Mwenyezi Mungu amlipe mema dokta fulani, alinihudumia hadi nikapona, alisema nini? Alisema: Nitakuhudumia hadi upone, huduma ni vitendo sio nadhariya (thiori).

Mambo haya manne kwa uchache kila anaye taka kutoa huduma anatakiwa ayazingatie.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: