Wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu imeipongeza mimbari ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kutoa huduma za kielimu katika fani mbalimbali zinazo lenga kuitumikia Iraq, na sisi tunawaunga mkona katika kufanikisha swala hilo.
Hayo yamesemwa katika ujumbe ulio wasilishwa kwa niaba ya wizara na Dokta Mussa Mussawi katika ufungaji wa semina ya chembechembe hai za ubongo, iliyo fanywa kwa ushirikiano wa Atabatu Abbasiyya na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, ujumbe huo unasema kua: “Ushirikiano na Atabatu tukufu hususan Atabatu Abbasiyya pamoja na wizara ya elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu vingine, ulianza kuongezeka tangu mwaka 2003, Ataba tukufu, hasa Atabatu Abbasiyya imekua ni sehemu za kufanyia makongamano na nadwa mbalimbali, na kuvialika vyuo vikuu kushiriki, na sasa wamejikita katika kiini cha elimu ambayo huongeza imani ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Akaongeza kua: “Nadwa hizi na harakati hizi zinasaidia sana wakufunzi wa vyuo vikuu vya Iraq, hakika mimbari ya Atabatu Abbasiyya imekuwa mstari wa mbele daima katika swala hili, sisi katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu tunathamini sana nadwa hizi na semina hizi zinazo toa elimu ya mambo mbalimbali, ikiwemo elimu ya tiba na uhandisi, tunaunga mkono swala hili na tupo tayali kuwasiliana na kila Ataba kwa ajili ya kusaidia harakati za aina hii”.
Akamaliza kwa kusema: “Hii ni semina maalumu iliyo jikita katika maswala ya tiba ya maradhi yanayo watesa watoto wengi wa Iraq ambayo ni maradhi ya upweke, Inshallah tutayafanyia kazi tuliyo soma katika semina hii, tunaviomba vyuo vikuu vyote kupitia vituo vyetu vya utafiti wafanye mazingatio maalumu ya maradhi haya na watafute njia za kujikinga nayo sambamba na kufanya tafiti tofauti, sisi katika wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, tunapongeza na kuthamini sana kazi hii inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa faida ya taifa la Iraq, wanafunzi wa Iraq na watoto wa Iraq, tunatarajia mafanikio mema kwa wanasemina wote”.