Qur’an tukufu ni tulizo la nafsi, inapo somwa roho huburudika na hupata utulivu kutokana na uzuri wa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hutia imani na utulivu katika nafsi, uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umekua mwenyezi wa hafla ya usomaji wa Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya na kwa ushiriki wa jopo la wasomaji kutoka mkoa wa Baabil kwenye tawi la Maahadi.
Hafla hii ni miongoni mwa harakati zinazo endelea kuratibiwa na kusimamiwa na Maahadi ya Qur’an ambazo zina sekta nyingi ikiwemo usomaji, waumini wamekusanyika kutoka katika mji wa Baabil na mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu wakisikiliza maneno matukufu ya kitabu hicho kisicho kua na shaka ndani yake.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Muhsin Rimahi, kisha ukafuata usomaji wa mahadhi murua ya kiiraq ulio somwa na Saahir Tamimi, halafu ikafuata kaswida iliyo somwa na Ahmadi Silawi iliyo elezea utukufu wa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), pazia ya usomaji wa Qur’an ikafungwa na bwana Hussein Khadhiir.
Kumbuka kua ofisi ya usomaji wa Qur’an katika Maahadi ya Qur’an inaendelea kufanya mahafali na vikao mbalimbali vya usomaji wa Qur’an, ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambapo hufanywa vikao vya usomaji Alasiri ya kila siku ya Ijumaa au katika mikoa mingine.