Mwaka wa kumi tangu kuanzishwa kwake: Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chafanya hafla na kuwazawadia wawakilishi wake na wafadhili wao…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya hafla kubwa ya kuadhimisha kumaliza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, iliyo fanyika Alasiri ya Juma Mosi (7 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (21 Julai 2018m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo hudhuriwa na viongozi wengi wa kitengo hicho pamoja na wawakilishi kutoka mkoa wa Karbala na mikoa mingine ya Iraq, na viongozi wengine mbalimbali na ujumbe ulio wakilisha pande tofauti.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa karbala, ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Shekh Ali Mujaan ambaye alizungumzia: “Umuhimu wa Imamu Hussein (a.s) na umuhimu wa kumuadhimisha, maadhimisho haya yamehimizwa na Maimamu wa Ahlulbait (a.s)”, akasisitiza kushikamana na maadhimisho hayo na kuongeza juhudi za kunyanyua sauti ya Imamu Hussein (a.s), katika maneno yake alitoa hadithi zinazo himiza swala hilo, ukizingatia kua kumpenda Imamu Hussein (a.s) na kuhuisha utajo wake ni miongoni mwa mafanikio ya safari ya hapa duniani.

Ukafuata ujumbe wa rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu bwana Riyadh Ni’imah Salmaan, alizungumzia mambo muhimu yaliyo fanywa na kitengo hicho ndani ya miaka kumi.

Wawakilishi ya kitengo pia walikua na ujumbe ulio wasilishwa na bwana Saadi Abdali ambaye ni kiongozi wa wawakilishi wa Diwaniyya, akasema kua: “Hakika maadhimisho ya Husseiniyya ni miongoni mwa turathi muhimu ya kidini na kitamaduni, ufanyaji wa maadhimisho hayo lazima uzingatie misingi ya dini na kusahihisha vitengo visivyo faa vinavyo weza kufanywa na wajinga au wanafiki”.

Hafla ilipambwa na filamu iliyo onyesha mambo muhimu yaliyo fanywa na kitengo hiki pamoja na vipande vya mashairi ya bwana Karaar Karbalai, mwisho kabisa wawakilishi wa kitengo kutoka Karbala na katika mikoa mingine wakapewa vyeti, pamoja na wawakilishi wa kikosi cha ulinzi wa malalo mawili matakatifu kilicho chini ya polisi wa mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: