Rais wa kitengo cha maadhimisho, mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu bwana Riyadh Ni’imah Salmaan ametaja mafanikio yaliyo fikiwa ndani ya miyaka kumi tangu kuanzishwa kwa kitengo hicho, ameyasema hayo katika hafla ya kuzima mshumaa wa kumi na kuwasha mshumaa wa kumi na moja iliyo fanyika Alasiri ya Juma Mosi (7 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (21 Julai 2018m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yafuatanyo ni mafanikio muhimu yaliyo patikana:
Kwanza: Kutokana na juhudi za pekee zilizo fanywa na kitengo hiki, kimeweka wawakilishi katika mikoa mingi ya Iraq wapatao (160) wanao simamia maadhimisho ya Husseiniyya katika wilaya na mitaa, wawakilishi hao walipatikana kupitia uchaguzi wa ndani na chini ya taratibu za kitengo hiki, wawakilishi hao wamesaidia kupunguza matatizo ya kipesa na kuratibu kazi za mawakibu Husseiniyya kiidara na kiutendaji, sambamba na kupewa ridhaa na Marjaiyya katika maadhimisho na mawakibu ya kila mkoa ibebe jukumu la kupangilia maadhimisho kiofisi, na kuwasiliana na serikali ya eneo baaba ya kupewa kila muwakilishi usimamizi kamili wa kiidara na nguvu ya kupangilia maadhimisho ya Husseiniyya.
Pili: Kuhakikisha kazi zote zinafanyika chini ya kivuli cha Imamu Hussein na maelekezo ya Marjaiyya bila kuingiza mambo ya siasa na matabaka.
Tatu: Kitengo kinapangilia ushiriki wa mawakibu zote za Husseiniyya za ndani na nje ya Iraq katika minasaba mbalimbali ikiwemo minasaba ya ziara za milionea (zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu), kutokana na aina ya maukibu kama ni ya kutoa huduma na ya kuomboleza, idadi ya maukibu za Husseiniyya zilizo sajiliwa ni zaidi ya elfu 29 za ndani na nje ya Iraq.
Nne: Kitengo hiki kilikua na nafasi kubwa katika kuhimiza mawakibu ziitikie fatwa ya kujilinda ya jihadi kifaya, kwa kufungua milango ya kutoa misaada ya aina mbalimbali kwa wapiganaji katika uwanja wa vita sambamba na kuwasaidia wakimbizi.
Tano: Kitengo kimesaidia kupunguza baadhi ya vitendo vya kikabila katika maadhimisho ya Husseiniyya.
Sita: Kitengo kimekua na mchango mkubwa katika kutangaza muhanga wa Imamu Hussein na kuufananisha na mazingira ya sasa, vyombo vya habari vya kiislamu ikiwemo luninga ya Karbala na mtandao wa kimataifa wa Alkafeel vimefanya kazi kubwa ya kutangaza matukio ya mimbari za Husseiniyya.
Akamaliza kwa kusema: “Tunawashukuru sana viongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa msaada wao endelevu na moyo wao wa kuhakikisha kua maadhimisho ya Husseiniyya yanakua taa linalo angaza katika kuwatumikia Ahlulbait (a.s), na njia ya kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) kwa namna bora, na shukrani za dhati ziwafikie watumishi wote wa Imamu Hussein (a.s)”.