Idara ya wahadhiri wa kike ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua semina ya uhadhiri kwa lugha ya kiengereza, ikiwa na washiriki zaidi ya wanafunzi sabini (70) walio faulu katika mitihani ya majaribio ya kujiunga na semina hiyo ambayo ilikua ya kuandika na kuongea ya kuangalia viwango vya elimu zao. Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike Ustadhat Taghriid Abdulkhaaliq Tamimi ameongea kuhusu semina hii kua: “Idara ya wahadhiri wa kike hufanya semina mbalimbali katika kipindi chote cha mwaka, kwa ajili ya kuandaa kizazi cha wahadhiri wa kike watakao fikisha fikra na mwenendo wa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), imesha toa wahitimu wengi ambao wana mchango mkubwa katika utowaji wa mihadhara (mawaidha) kwenye matukio (minasaba) mbalimbali, na wameweza kufundisha wahadhiri wengine, kwa ajili ya kuendana na maendeleo ya sasa yaliyopo katika fani ya uhadhiri wa wanawake, na umuhimu wa kuwa na wahadhiri wa lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya kiengereza, tumeamua kuandaa semina kwa lugha ya kiengereza, hii ni semina ya kwanza ya aina hii kufanywa na taasisi ya wahadhiri wa kike, tena kwa kufuata selebasi iliyo andaliwa kwa ustadi mkubwa chini ya usimamizi wa kamati ya wataalamu itakayo zaa wahitimu wenye uwezo mzuri wa kutoa mihadhara kwa lugha ya kiengereza”.
Akaongeza kua: “Mwitikio wa kushiriki katika semina hii ulikua mkubwa sana, lakini kutokana na udogo wa eneo pamoja na kuhakikisha wanapewa elimu kwa urahisi, tumetosheka na idadi hii ya washiriki zaidi ya (70) na wengi wao ni wanafunzi wa vyuo wanao somea lugha ya kiengereza, tuliandaa mtihani wa majaribio wa kuingia katika semina hii, tunatarajia kuendelea kufanya semina zingine katika siku za usoni kwa lugha ya kiengereza au lugha nyingine”.
Msimamizi mkuu wa semina hii Shekh Amiir Yasini Waliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Aina hii ya semina ni mara ya kwanza kufanyika, tuliangalia idadi ya washiriki na viwango vyao vya elimu, tukakuta asilimia kubwa ni wahitibu wa shahada ya bachela katika vyuo mbalimbali, baada ya kuwapa mtihani wa majaribio wanafunzi walio faulu walikua wanakaribia (80), na semina itakua na mafanikio kwa sababu wanafunzi wana hamasa kubwa, na tutaandaa walimu walio bobea katika fani hii, tumesha andaa selebasi inayo endana na viwango vya elimu za wanafunzi hawa ambayo inajumuisha mambo mengi”.