Kwa vikosi vitatu: Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaimarisha ulinzi katika njia (barabara) ya kwenda hijja…

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza kuimarisha ilinzi katika njia ya kwenda hijja kupitia nchi kavu baina ya Iraq na Saudia (Nakhibu – Ar-ur) kwa vikosi vitatu kikiwemo kikosi cha deraya, baada ya kupokea maagizo kutoka kwa viongozi wa bulgedi ya Furaat katika kikao kilicho fanyika mwezi huu makao makuu ya kikosi.

Uongozi wa kikosi cha Abbasi umesema kua, wanatarajia kumaliza kusambaza vikosi vya deraya ndani ya mwezi ujao wa Agosti, katikati ya mwezi huo inatarajiwa kuanza misafara ya kwenda hijja kupitia njia kavu (barabara) wakiingilia mji wa mpakani wa Ar-ur chini ya usimamizi wa taasisi za hijja na Umra za Iraq.

Kamanda wa kikosi cha nne (kikosi cha Imamu Ali –a.s-) Sayyid Abbasi Abu Twabiikh amesema kua, kikosi kimepokea taarifa za kwanza kutoka kwa kamati ya hijja na umra ya Iraq ndani ya wiki hii ambao wamekamilisha maandalizi ya kuwahudumia mahujaji wanao kwenza katika nyumba tukufu.

Naye Ali Hussein Nashami ambaye ni kamanda wa kikosi cha tatu (kikosi cha Ummulbanina –a.s-) kua kikosi kimekamilisha maandalizi katika kituo cha mji wa Nakhibu ya kuwapokea mahujaji katika eneo la mapumziko, kwa ajili ya kusubiri maelekezo kutoka kwa viongozi wa kamati ya hijja na kupewa huduma.

Tunapenda kusema kua sehemu ya wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) wanalinda amani katika mji wa Nakhibu tangu miaka mitatu chini ya usimamizi wa bulgedi ya Furaat na haijawahi kutokea uvunjifu wa amani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: