Maandalizi ya uwekaji wa marumaru: kumalizia ujenzi wa chini katika uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza kazi zote za ujenzi wa chini katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuandaa uwekaji wa marumaru mpya zitakazo anza kuwekwa baada ya kumaliza uwekaji wa marumaru katika haram tukufu.

Kazi za mradi huu zimepitia hatua tofauti, baada ya kupata michoro na ramani ya mradi huu, kazi ilianza mara moja, ilihusisha utengenezaji wa mtandao mpya wa njia za maji ya mvua na maji ya kuoga ndani ya haram tukufu na ukachukua nafasi ya mtandao wa zamani, na kuunganisha mtandao huo na mtandao mkuu wa Ataba tukufu.

Baada ya kuondoa marumaru za zamani lilichimbwa shimo kwa ajili ya kuweka mabomba yenye upana wa sm90 na urefu unao endana na ukuta wa ndani wa uwanja wa haram tukufu, katika eneo linalo kadiriwa kwa na 2m433 baada ya kuweka tabaka la chuma katika sehemu ya shimo kwa viwango maalumu vilivyo pasishwa na wahandisi, na kuweka njia za maji 40 zilizo sambaa katika eneo lote kwa viwango maalumu, kwa ajili ya kuweka mabomba bora kabisa ya kisasa yanayo endana na mahitaji ya uwanja mtukufu wa haram, kwa kweli mabomba hayo yanakubali kufungamana na kitu kingine, kama vile umeme na vinginevyo, kisha wakaweka mabomba chini kwa kufuata vipimo vya sakafu na makadirio ya uwekaji wa marumaru.

Kumbuka kua uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia miradi mingi iliyo tekelezwa kila mmoja kwa wakati wake maalumu kutoka na aina ya mradi, kama vile mradi wa upanuzu wa haram kwa upana na urefu, upauwaji wa uwanja wa haram tukufu, uwekaji wa vifuniko kajika sehemu za jengo la Ataba, ujenzi wa sardabu zilizopo katika haram, utengenezaji na uwekaji wa dirisha tukufu, sambamba na uwekaji wa mifumo mbalimbali, kama vile mfumo wa viyoyozi, zima moto, utowaji wa tahadhari, mawasiliano, ulinzi na mingine mingi, nafasi haitoshi kuelezea yote, mtiririko wa miradi hiyo unahitimishwa na mradi huu wa kuweka marumaru katika uwanja wa haram tukufu, kwa mara ya mwisho mradi huu ulifanywa katika miaka ya sabini karne iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: