Darsa hizi hufanywa kila wiki kwa muda wa saa tatu katika kituo kikuu cha Swidiqah Twahirah (a.s) kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya, darsa hizi zilianza mwanzoni mwa likizo za kiangazi kwa ajili ya kuutumia kwa faida muda wa likizo, zimepata mwitikio mkubwa na washiriki wengi baada ya kutangazwa kwa program hii yenye vipengele vingi vikiwa na lengo la kuandaa kizazi chenye maadili mema ya kiislamu yanayo wawezesha vijana kupambana na changamoto zote za kifikra zinazo lenga kuharibu umma hususan tabaka la vijana, ratiba inamasomo yafuatayo:
- - Kujifundisha Qur’an usomaji wa tukufu.
- - Tafsiri ya baadhi za aya za Qur’an zinazo husiana na hali halisi ya maisha ya sasa.
- - Kusherehesha mambo ya kifiqhi na kiaqida.
- - Maadili kwa ujumla.
- - Mihadhara elekezi.
- - Vipindi vya mapumziko (burudani).