Hapa ndio ulipo fikia utengenezaji wa mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ujenzi na matengenezo yanayo endelea katika Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo ongeza uzuri wa jengo hili tukufu, ni mradi wa upanuzi wa mlango wa Kibla wa malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), matengenezo yanaendelea katika mlango wa Kibla wa malalo matukufu, matengenezo ya hali ya juu katika ufundi na uhandisi wa majengo yanayo ufanya mlango huo kuwa wa pekee, yamekamilika matengenezo muhimu hivi karibuni na baadhi ya kazi zimeanza kuonekana bayana, pamoja na kwamba unahitajika umakini mkubwa katika utekelezaji wa mradi huu pia unahitajika muda wa kutosha, kwa ujumla kazi inaendelea vizuri kwa wakati na kwa ubora ulio tarajia, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mlango wa Kibla unahadhi kubwa katika nyoyo na akili za mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s),hili ndio lililo tupelekea tuupe kipawa mbele zaidi tofauti na milango mingine ambayo imetengenezwa kwa viwango vya juu pia, kazi za matengenezo katika mlango huo zinaendelea vizuri kama zilivyo pangwa hatua moja baada ya nyingine, kuna hatua zingine zinachanganywa mbili kwa wakati mmoja ili kuharakisha utendaji, tayali kazi wa uwekaji wa marumaru za mapambo chini ya mduara wa mlango wa Kibla imesha anza, ni vipande vya marumaru vya mstatiri vimechorwa mapambo ya mimea na michoro mingine ya kiufundi na mizuri sana, inayo endana na nakshi zilizopo, sawasawa ziwe zile za kasha au zinginezo zenye muonekano mzuri, mapambo hayo yamewekwa upande wa kulia na kushoto ya mlango, kazi hiyo ilitanguliwa na uwekaji wa vifuniko maalumu ambavyo juu yake ndio zinawekwa marumaru hizo za mapambo”.

Akabainisha kua: “Hali kadhalika tumemaliza uwekaji wa mapambo makuu ya upinde ambayo yapo matatu yaliyo tiwa dhahabu halisi, yamenakshiwa kwa herufi za Qur’an, pinde hizo zimeungana na ufito wa dhahabu unao zunguka juu ya mlango kwa ndani, hali hiyo hiyo ipo pia kwa nje, kazi hii imefanyika sambamba na kazi nyingine ya uwekaji wa kashi kwa ndani”.

Akaendelea kusema: “Dari la eneo la mlango ambalo lenyewe tu ni pambo tosha, tumemaliza uwekaji wa tabaka ya chuma maalumu kinacho kubali kuwekwa nakshi na mapambo mbalimbali, nayo ni kazi kamili iliyo tumia aina maalumu za vyuma vinavyo endana na mambo yatakayo wekwa juu yake, kuanzia uzito na aina pamoja na mambo mengine, zimezingatiwa tahadhari mbalimbali za kiufundi, kazi imekamilika kwa kiasi kikubwa na tumeanza kuweka kashi karbalai zenye ufito wa dhahabu”.

Kumbuka kua mradi huu upo ndani ya mradi mkubwa ambao ni upanuzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ndio imeonekana haja ya kupanua milango na kuifanya kua ya kisasa maradufu zaidi ya ilivyo kua awali, kwa kuweka nakshi na mapambo mbalimbali, kila mlango unatengenezwa na kupambwa kulingana na nafasi ya mlango husika, ili iweze kuhimili idadi kubwa ya mazuwaru na mawakibu (vikundi) vya Husseiniyya ambavyo huingia ndani ya Ataba tukufu, milango hii imesanifiwa na kutengenezwa na shirika la ujezi la Ardhi tukufu chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Ataba tukufu, kutokana na namna ilivyo tengenezwa milango hii na namna ilivyo pambwa hakika ilikua inahitaji muda mrefu unao endana na kazi hizi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: