Imeangaza nuru ya mtoto mtukufu*** Mtoto wa Nabii Mustafa Adnani.
Wasii wa Ahmadi Nabii mtakatifu*** Kwa akili na nakili na Qur’ani.
Imamu wa nane mtakasifu*** Muongoaji wa viumbe wote wa Rahmani.
Muokozi wetu siku ya kiyama*** Katika swiratwa pia katika mizani.
Nyoyo zinaelekea katika Ataba tukufu zikiwa safi, zimejaa mapenzi ya Imamu Ridha (a.s), jua la uongofu utokanao na Imamu Ridha (a.s) limechomoza, na dunia imevaa joho la shangwe na furaha, zimekutana furaha za Malaika na viumbe wote, kwanini isiwe hivyo wakati umezaliwa mwezi wa Muhammadiyya wa nane miongoni mwa nuru za Alawiyya Imamu Ali bun Mussa Ridha (a.s), ambaye alizaliwa siku kama ya kesho Juma Tano (11 Dhulqa’ada).
Furaha imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, vitengo vya Ataba vimefanya kazi ya kuweka mapambo yanayo endana na furaha hii, yamewekwa mabango na kufungwa taa nzuri katika milango na kila mahala ndani ya uwanja wa haram tukufu, mabango mbalimbali yenye hadithi na maneno ya hekima kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) yamewekwa katika kuta za uwanja wa haram tukufu.
Yote hayo yamefanyika kutokana na athari kubwa ya tukio hili kwa waislamu wote, wanaokuja kumpongeza Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na mnasaba huu.