Mwezi wa dhulqa’ada una matukio mengi, kubwa ni hili la kuzaliwa kwa Imamu wa nane miongoni mwa Maimamu wa kizazi kitakatifu cha Mtume Muhammad mbora wa walimwengu, ambaye ni Abulhassan Ali Bun Mussa Ridha (a.s) (Shamsi Shumusi wa Anisi Nufusi Almadfunu bi-ardhi Tusi). Tarehe kumi na moja mwezi kama huu wa (Dhulqa’ada) mwaka wa (148h) katika mji wa Madina, nuru iliangaza katika ardhi kwa kuzaliwa Imamu Mtakatifu, shangwe na furaha ilijaa katika nyumba ya Imamu Mussa bun Jafari (a.s), wafuasi wake wakajaa katika nyumba hiyo tukufu ambayo Mwenyezi Mungu ameagiza iheshimiwe na litajwe jina lake ndani ya nyumba hiyo, ardhi na mbingu vilinawirika kwa kuzaliwa mbora wa watu wa duniani Imamu Ali bun Mussa Ridha na akaitwa Murtadha (a.s), mama yake ni Ummu Walad na jina lake ni (Tuktam) na inasemekana anaitwa (Najma) alikua mwanamke bora zaidi mwenye akili sana na mshika dini, Imamu Alkadhim (a.s) alikua anamwita kwa jina la Mtakasifu (Twahira).
Kutoka kwa Shekh Swaduqu katika mapokezi yanayo ishia kwa Ali Bun Maitham kutoka kwa baba yake, anasema: Nilimsikia mama anasema: Nilimsikia Najma mama wa Imamu Ridha (a.s) anasema: “Nilipo pata ujauzito wa mwanangu Ridha, sikupata tabu yeyote ya ujauzito, na nilikua ninapo lala nasikia tasbihi, tahlili na tamjidi tumboni mwangu, jambo hilo lilikua likinishtua, nikiamka sisikii kitu, siku ya kumzaa, alitoka na kuweka paji la uso wake katika ardhi na akainua mikono yake juu akawa anachezesha midomo yake kama vile mtu anaye ongea, akaingia baba yake Mussa bun Jafari (a.s) akaniambia: Hongera sana ewe Najma, Mwenyezi Mungu amekukirimu”, nikampa mtoto akiwa katika kitambaa cheupe, akamchukua na kumuadhinia katika sikio lake la kulia halafu akakim katika sikio lake la kushoto, kisha akachukua maji ya mto Furat akamuwekea mdomoni, halafu akamrudisha kwangu, akaniambia: Mchukuwe ewe Najma hakika huyu ni alama ya Mwenyezi Mungu iliyobakia katika ardhi”.
Imeangaza nuru ya mtoto mtukufu *** Mtoto wa Nabii Mustafa Adnani.
Wasii wa Ahmadi Nabii mtakatifu *** Kwa akili na nakili na Qur’ani.
Imamu wa nane mtakasifu *** Muongoaji wa viumbe wote wa Rahmani.
Kuzaliwa kwake (a.s) ukawa ni ukurasa mpya wa kheri na uongofu, alikua (a.s) ni kiongozi muokowaji katika kimbunga cha fitina, matamania na mmomonyoko wa maadili, huyu ni wa nane katika maimamu wa nyumba ya Mtume watakasifu (a.s), imebarikiwa siku aliyo zaliwa, na watu wote wamebarikiwa kwa kupewa tunu hii tukufu, Mwenyezi Mungu atuwezeshe kumtembelea hapa duniani, na atupe shifaa yake kesho akhera, na hiyo ndio neema kubwa na kufaulu, amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uawa kwa sumu na siku atakayo fufuliwa na kuwa hai.