Mradi wa majengo ya shule wa awamu ya pili wapiga hatua kubwa…

Maoni katika picha
Kazi ya ujenzi inasonga mbele katika mradi wa ujenzi wa shule wa awamu ya pili, amboa ni miongoni mwa miradi muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimkakati, nisehemu ya muendelezo wa mradi wa kwanza na wa tatu, mradi huu unahusisha ujenzi wa shule za wavulana na wasichana pamoja na shule za awali (chekechea) na ukumbi wa michezo pamoja na vitu vingine, unajengwa kwa kiwango kizuri zaidi kinacho endana na lengo la ujenzi huo, majengo hayo yatakua mahala bora pa kusoma na kupata malezi mazuri ya kielimu na kitamaduni yatakayo wanufaisha zaidi wahusika.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandiri Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inaipa umuhimu mkubwa miradi maalumu pamoja na hali ngumu ya pesa inayo likumba taifa kwa ujumla na kuathiri utendaji wa miradi kama hii, kutokana na umuhimu wake imekua vigumu kuichelewesha au kuiacha kabisa, ukiwemo mradi huu wa shule, tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha mradi unaendelea”.

Akaongeza kua: “Tuna mshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu, mradi unaendelea vizuri ndani ya muda ulio pangwa na ubora ulio tarajiwa, ujenzi umefika mahala pazuri pamoja na ugumu wa mazingira ya upatikanaji wa pesa, tayali kazi zote muhimu zimekamilika, kama vile ujenzi katika maeneo ya kuweka zege, na kuweka mifumo ya (Umeme, maji, vyoo, zima moto, onyo, mawasiliano, intanet na kamera) kazi ya kuweka milango na madirisha imesha anza pamoja na kupiga ripu katika baadhi za kuta zilizo kamilika, maandalizi ya kazi zote yako vizuri na kazi zinaendelea bila kusimama”.

Kumbuka kua mradi wa jengo hili upo katika barabara ya (Karbala – Hilla) katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m10,710), unajumuisha shule mbili za wavulana zenye kumbi za madarasa na maabara pamoja na vitu vingine muhimu katika elimu, jengo lina ghorofa tatu, eneo la shule ya awali (chekechea) linaukubwa wa mita za mraba (1,250) nayo ni ya ghorofa tatu na kuna ukumbi wa michezo wenye matumizi mbalimbali, unaukubwa wa mita za mraba (1300), pia kuna shule nyingine wa wasichana, kila shule inajengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (2,400), zote zinajengwa kwa viwango vya kisasa vinavyo endana na matumizi ya vifaa vya kisasa katika kila kitu, pamoja na kuzingatia uwiyano wa shule hizi na zile za kwanza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: