Mkuu wa Maahadi ya turathi za Mitume: Mbele yetu kuna kazi ya kunukuu maarifa ya Ahlulbait (a.s) kwa kutumia kila chombo kinachoweza kuyafikisha kwa walimwengu…

Maoni katika picha
Katika hafla iliyo fanywa na Maahadi ya turathi za Mitume inayo toa masomo ya hauza kwa njia ya mtandao chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuanza mwaka mpya wa masomo, iliyo fanyika Alasiri ya Alkhamisi (12 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (26 Julai 2018m) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu, kulikua na ujumbe ulio tolewa na mkuu wa Maahadi Shekh Hussein Turabiy usemao kua:

Yatupasa kutafakari kwa kina kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa akiyafanya). Aya hii inaonyesha wazi kua watu tupo makundi mawili:

Kundi la kwanza: Ni watu wenye uhai wa kudumu haukatishwi na kifo cha duniani, wako chini ya usimamizi wa Mwenyezi Mungu, amewapa ulinzi, hawasombwi na mafuriko wala hawapeperushwi na kimbunga, hawayumbishwi na shida wala misukosuko, wamezama katika mapenzi ya Mola wao kiasi kila kinacho wasibu wao hukiona ni kizuri na kinawazidisha utulivu, wana amani na usalama hawana hofu wala wasiwasi, wanaishi hivyo bila kutetereka umri wao wote.

Kundi la pili: Ni watu waliotoka katika usimamizi wa Mwenyezi Mungu, wanaishi wakiwa katika giza bila nuru ya imani, wamezama katika giza na hawana pakutokea, wana giza la kifo, giza la ujinga katika kupambanua mambo, hawajui jambo la kheri wala la shari, lenye manufaa au madhara.

Akaongeza kua: “Hiyo ndiyo hali ya mwanadamu kabla hajapata uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu huwa sawa na maiti asiye kua na neema za uhai, hana hisia wala wawezi kutenda jambo, na tukitafakari maneno ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) tutaona ukweli uko wazi, hakika uhai wa mwanadamu unategemea elimu na maarifa, na njia ya kupata uongofu wa Mwenyezi Mungu inapatikana kwa kusoma na kupata maarifa ya kweli, na sisi tumesimama hapa leo kama tulivyo simama jana kwa ajili ya kupongeza kundi jipya la wanafunzi watukufu walio jiunga na safari hii ya kutafuta elimu.

Wamejiunga kupitia maendeleo ya mawasiliano tuliyo nayo leo, baada ya kushindwa kujiunga moja kwa moja katika hauza na vituo vya elimu, wametumia vizuri fursa hii ya mawasiliano na wamejitolea muda wao na kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kutafuta elimu, hakika wamepoza kiu yao kwa kuitafuta elimu katika chemchem safi na vyanzo asili vya elimu katika hauza za Najafu chini ya nuru za Alawiyya na huduma za Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Tunatoa pongezi kubwa kwa wanafunzi wetu wakike na wakiume, pia tunawapongeza wakina dada walio kubaliwa kujiunga na chuo cha Ummul Banina cha kimtandao, kinacho andaa wahubiri wa kike (mubalighati), chuo ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kuitikia maombi ya jamii katika sekta ya tablighi, ili kuandaa wahubiri bora wa kike wenye uwezo mzuri wa kufikisha ujumbe wa kiislamu kielimu, chuo hiki kinatumia selibasi ya hauza iliyo andaliwa na maustadhi walio bobea katika masomo ya hauza katika mji mtukufu wa Najafu, chuo hiki kinatoa mafunzo kwa kufuata mfumo wa Maahadi kwa kutumia intanet (elimu masafa) na sio moja kwa moja”.

Turabiy akaendelea kusema kua: “Leo tumekutana kuwapongeza wanafunzi walio faulu na walio kubaliwa kujiunga na chuo, tunamuomba Mwenyezi Mungu awape taufiqi katika maisha yenu, mimi sichukulii hafla hii kuwa ndio mwisho, bali huu ni mwanzo, mbele yetu kuna kazi kubwa, mbele yetu kuna kuongea na mataifa mbalimbali kuhusu ukweli wa utukufu wa dini yetu takatifu, na mbele yetu kuna kazi ya kunukuu maarifa ya Ahlulbait (a.s) katika kila chombo kinacho weza kuyafikisha kwa walimwengu yakiwa katika hali ya kusomwa, kusikilizwa na kuangaliwa
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: