Maahadi ya turathi za Mitume yawapongeza wanafunzi walio faulu katika kiwango cha Tamhidi na yaanza mwaka mpya wa masomo kwa kutoa zawadi kwa washindi wa mashindano waliyo endesha…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridha (a.s) Maahadi ya turathi za Mitume inayo toa masomo ya hauza kwa njia ya mtandao (elektronik) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imewapongeza wanafunzi walio faulu katika hatua ya tamhidi, na imetangaza kuanza kwa mwaka mpya wa masomo, pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi walio faulu katika mashindano waliyo endesha, sambamba na kutoa zawadi kwa wanafunzi wa kike walio kubaliwa kujiunga katika chuo cha Ummul Banina (a.s) cha kuandaa mubalighati (wahubiri wa kike), hayo yamefanyika katika hafla ya kumaliza mwaka wa tatu kwenye ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, ikafuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukafuata wimbo wa Ataba tukufu, kisha ukafuata ujumbe wa Ataba ulio wasilishwa na rais wa kitengo cha dini Shekh Swalahu Karbalai, ambaye alipongeza juhudi nzuri za wanafunzi zilizo wawezesha kupata mafanikio haya, akawasisitiza kuendelea kufanya juhudi katika kutafuta elimu ya dini na kupata maarifa zaidi, pia aliwasifu wasimamizi wa Maahadi, walimu pamoja na viongozi kwa juhudi zao za kufikisha elimu kwa wanafunzi.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa mkuu wa Maahadi ya turathi za Mitume na masomo ya hauza kwa njia ya mtandao Shekh Hussein Turabiy ambye amesema kua: “Mbele yetu kuna kazi kubwa, mbele yetu kuna kuongea na mataifa mbalimbali kuhusu ukweli wa utukufu wa dini yetu takatifu, na mbele yetu kuna kazi ya kunukuu maarifa ya Ahlulbait (a.s) katika kila chombo kinacho weza kuyafikisha kwa walimwengu yakawa katika hali ya kusomwa, kusikilizwa na kuangaliwa…”

Halafu ukafuata ujumbe wa wakufunzi ulio wasilishwa kwa niabaya yao na Shekh Hussein Abduridha Asadiy, ambaye alisema kua: “Hakika elimu ni nyingi sana haina mwisho, jambo hili kalitaja Mwenyezi Mungu mtukunfu pale alipo sema: (Na juu ya kila mwenye elimu kuna mwenye elimu zaidi), ni kosa mwanafunzi kuridhika na elimu aliyo nayo, bali anatakiwa awe na kiu ya kuendelea kusoma zaidi, mtu anapo fikia mahala akaona ndio mwisho wa elimu yake hakika hapo ndio huwa mwanzo wa ujinga wake, elimu inaviwango visivyo isha, wakati wote utakutana na mtu mwenye elimu zaidi yako, ni kosa pia mtu yeyote kujivunia elimu aliyo nayo au shahada alizo nazo au vitabu alivyo andika, hakika elimu ni sawa na kitu fulani cha kukufukisha katika lengo fulani ambalo ni muhimu kwa muumini kulifikia lengo hilo, pia elimu peke yake haitoshi kumfanya mtu aishi vizuri”.

Mwisho wa hafla hiyo wanafuzi walio faulu hatua ya tamhidi wakapewa zawadi pamoja na wale walio shinda katika mashindano yaliyo endeshwa na Maahadi, vilevile wakapewa zawadi wanafunzi wa kike walio kubaliwa kujiunga katika chuo cha Ummul Banina (a.s) cha kimtandao kinacho andaa wahubiri wa kike (mubalighati).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: