Marjaa dini mkuu atoa maelekezo kwa serikali ijayo na kama isipo tekeleza iliyo ahidi raia hawatakua na chagua lingine zaidi ya kuendelea na maandamano ya amani wakati huo hali itakua na picha nyingine tofauti na ilivyo leo…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu ameonyesha njia ya kuunda serikali ijayo haraka iwezekanavyo chini ya misingi sahihi na watu wenye uwezo wasio kuwa na tuhuma, waziri mkuu awajibike kikamilifu katika utendaji wa serikali yake, iwe serikali yenye nguvu itakayo pinga ufisadi na ubadhirifu ambavyo ndio msingi wa matatizo yanayo likumba taifa leo, hilo ndio liwe jukumu lake la kwanza na jukumu la msingi, awapige vita mafisadi na kila anaye walinda, na serikali iahidi kufanya kazi kwa haki na uadilifu chini ya kanuni zinazo eleweka, ikiwa ni pamoja na:

Kwanza: Kuwasilisha bungeni mapendekezo ya kubadilisha kanuni zinazo toa haki kwa watu fulani na kuwanyima haki hiyo wengine bila kujali usawa baina ya raia.

Pili: Kuwasilisha bungeni mapendekezo ya kanuni zinazo toa mwanya kwa mafisadi na ambazo wamekua wakizitumia kufikia malengo yao, na kuunda mamlaka ya kupambana na ufisadi.

Tatu: Kuwe na kanuni imara zitakazo tumika katika uteuzi wa mawaziri na nafasi zingine za juu serikalini, kuwe na vipengele vinavyo mzuwiya kushika nafasi hizo asiye kuwa na sifa fulani, na mwenye kutuhumiwa kwa ufisadi, na mtu anaye wagawa raia kwa msingi wa madhehebu zao au vyama vyao vya kisiasa, na mtu anaye tumia mali za serikali kwa manufaa binafsi, au kwa faida ya rafiki zake au chama chake na mengineyo mfano wa hivyo.

Nne: Kuipa nguvu taasisi ya kusimamia mali za serikali, na kufanyika ukaguzi wa hesabu za mwisho wa mwaka katika bajeti za serikali katika kila kitu na katika wizara zote na mikoa yote, na matokea ya ukaguzi huo yatangazwe hadharani ili kuwatambua walio fuja mali za serikali na walio fanya uzembe sambamba na kuchukua hatua kwa walio fanya ufisadi, bunge lijalo linatakiwa lifanye kazi kwa makini na lichukue hatua za kurekebisha, pamoja na kupitisha kanuni zitakazo wasaidia kuleta maendeleo ya taifa, iwapo serikali haitafanya jambo ililo ahidi au bunge likakwamisha jambo fulani au mahakama, raia hawatakua na chaguo lingine zaidi ya kuendelea na maandamano yao ya amani ili kuwasilisha madai yao kwa viongozi wakiungwa mkono na kila mwenye uchungu na taifa, wakati huo hali haitakua kama ilivyo, itakua na picha nyingine, tunatarajia hali isifike huko kiasi akili haita fanya kazi na kauli haita faa, hakika kutengemaa kwa taifa kupo mikononi mwa viongozi wao ndio wenye maamuzi wafanye hima kurekebisha mambo kabla muda haujaisha, na Mwenyezi Mungu ni muwezeshaji wa mazuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: