Wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu imetoa amri ya kikipandisha hadhi (chuo cha Alkafeel) kilichopo katika mkoa wa Najafu chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kuwa (Chuo kikuu cha Alkafeel) chenye vitivo vifuatavyo: (kitivo cha udaktari wa meno, ufamasiya, sheria, uhandisi na tiba na afya), hatua hii imechukuliwa baada ya kushuhudiwa mafanikio ya miaka kadhaa ya kiutendaji na kiuongozi katika chuo cha Alkafeel, na yote hayo yametokana na msaada endelevu kutoka kwa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Chuo hiki kimekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza elimu na utafiti katika nchi yetu kipenzi.