Tukio la aina yake hapa Iraq: Kituo cha Ummul Banina (a.s) Alkhairiyya kinacho jihusisha na tiba ya meno chaendesha mradi wa kibinadamu…

Maoni katika picha
Kituo cha Ummul Banina (a.s) Alkhairiyya cha tiba ya meno chaendesha moja ya miradi ya kibinadamu chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, unao lenga kutoa huduma za lazima kwa watoto yakiwemo matibabu, kadri ya uwezo wao katika kutekeleza hilo, lengo kubwa katika mradi huu ni kutoa elimu kuhusu utunzaji wa meno, na kuweka kifaa maalumu kwa ajili ya ulinzi wa meno sambamba na kutoa msaada wa matibabu ya meno kwa watoto.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kitengo cha meno Ustadh Ali Bahadeli, amesema: “Kituo kinafanya jambo hili kwa mara ya kwanza hapa Iraq ni jambo muhimu sana katika ulinzi wa meno, linalenga watoto wenye umri kati ya miaka (6 hadi 12) kutoka mikoa yote ya Iraq, kipawa mbele zaidi wanapewa mayatima na watu wanao ishi katika mazingira magumu, kwa kuwasiliana na taasisi pamoja na ofisi za Maraajii dini, katika mkoa wa Karbala tumepokea mamia ya watoto na tukoa matibabu, na kutokea hapo tunaelekea katika mikoa mingine chini ya ratiba iliyo pangwa.

Akaongeza kua: “Hakika kituo kinatoa huduma bure, madaktari na wauguzi wanaotoa huduma wanajitolea, na ni wataalamu walio bobea katika sekta hiyo, wanatoka ndani na nje ya Iraq, Atabatu Abbasiyya tukufu inawapa makazi na usafiri pamoja na vifaa tiba vilivyopo kituoni, ambavyo vina ubora mkubwa”.

Akabainisha kua: “Kituo kina vifaa bora kutoka (Italia) vinavyo kiwezesha kutoa huduma nzuri zinazo kubalika kimataifa, kituo kina idara nyingi, idara ya meno, idara ya mionzi na zinginezo, kituo kina madaktari bingwa na kinafanya kazi saa (7) kila siku”.

Pamoja na huduma nzuri zinazo tolewa na kituo, kitu bora zaidi kituo hiki ni kituo cha Khairiyya (kutoa misaada), na kina watu walio bobea katika fani mbalimbali ikiwemo tiba ya meno na namna ya kuyalinda yasidhurike.

Muuguzi mmoja bwana Ali Naatwiq –Mganga msaidizi anayefanya kazi katika kituo hicho- amesema kua: “Kituo hiki mwanzoni kilikuwa kinatibu watoto wa Karbala peke yake, kisha kikaanza kutibu watoto wa mikoa ya jirani na Karbala, na tunatoa kipau mbele zaidi kwa mayatima (mayatima wa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi), wanaokuja binafsi au kutokea katika taasisi au shule, tunatumia njia ya kuhamasisha, tunapo mpokea tunamtoa hofu na kumpa matumaini halafu ndio tunampeleka katika hatua ya matibabu”.

Kumbuka kua kituo hiki kipo ndani ya chuo kikuu cha Ameed, kilichopo katika barabara ya (Najafu – Karbala), utekelezaji wa umradi huu unatokana na moyo wa Atabatu Abbasiyya tukufu na uwajibikaji wao wa kimaadili unao sukumwa na utukufu wa mwenye malalo hiyo takatifu Abulfadhil Abbasi (a.s), pia kutokana na uchache wa vituo vya wataalamu wa meno, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kuanzisha kituo cha meno cha watoto.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: