Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto ya Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa ratiba yake ya mafunzo ya kujenga uwezo kwa wanaskaut wenye umri wa miaka (13 hadi 15), imefungua uwanja wa mihadhara ya Aqida na Akhlaq, kutokana na umuhimu wa mada hizo katika kujenga vijana wa umri huo.
Ustadh Samad Saalim kiongozi wa idara ya watoto na makuzi ametuambia kua: “Ratiba hii imeanza wakati wa likizo za kiangazi kwa ajili ya kuhakikisha tunatumia vizuri fursa ya kipindi cha likizo, ina vipengele vingi, kikiwemo kipengele hiki cha mihadhara inayo tolewa katika ukumbi wa chuo cha Ameed na kushiriki wanaskaut (200), inaendelea kwa muda wa siku nne, kila siku saa tatu zinazo gawanywa sehemu mbili, mihadhara hiyo inamada kuu tofauti, kuna mada ya: mpangilio wa maisha, Aqida, kuthibitisha uwepo (wa Mwenyezi Mungu), uadilifu wa Mwenyezi Mungu, utume, uimamu na kiyama. Kuhufu upande wa malezi kuna mada za: vitendo vyema, namna ya kujiepusha na dhambi na athari za tabia katika maisha ya mwanadamu. Wameshiriki mashekhe mbalimbali katika utowaji wa mada hizo, kila mmoja alizungumza kutokana na fani yake”.
Kumbuka kua ratiba ya kujenga uwezo ya hatua ya pili imeboreshwa, ni ratiba nzuri inayo husisha mambo mbalimbali ikiwemo mihadhara ya mada tofauti pamoja na masomo ya nadhariya na vitendo katika sekta zote, inaongeza uwezo wa vipaji vya washiriki na kukuza fikra zao.