Mbeba bendera wa kubba lake takatifu: Ugeni kutoka katika malalo ya Imamu Ridha (a.s) wapamba mradi wa Arshi Tilawa katika hafla ya mwisho wa wiki…

Maoni katika picha
Mradi wa Arshi Tilawa unaendelea -ambao ni moja ya miradi inayo endeshwa na kituo cha kuandaa wasomi wa Qur’an kilicho chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya- na vikao vya usomaji wa Qur’an vya kila wiki, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ridha (a.s) ambayo bado harufu yake inaendelea kunukia, wiki hii mradi umepata ugeni kutoka katika malalo ya Imamu Ridha (a.s) ukiwa na bendera ya kubba lake tukufu.

Umepambwa na wasomaji mahiri walio soma kwa vikundi na kuburudisha masikio ya wahudhuriaji pamoja na kukonga nyoyo zao, wahudhuriaji na mazuwaru wamenufaika na usomaji wa Qur’an wenye ushiriki mkubwa, yalitanda mazingira mazuri ya Qur’an yaliyo ungana na pumzi za Abulfadhil Abbasi (a.s), katika mahafali hiyo ya Qur’an tukufu, msomaji wa Atabatu Radhawiyya mwana Muhammad Ghiyashi alisoma pia na mwisho akasoma mtumishi wa Ahlulbait (a.s) Mula Ammaar Alkinani kisha zikasomwa beti za mashairi kwa sauti nzuri kwa ajili ya kuonyesha furaha ya tukio hili tukufu.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya inamiradi mingi ya Qur’an, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi huu wa Arshi Tilawa, nao unalenga kunufaika na vipaji vya wasomaji wa kiiraq na kuvionyesha katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kuangalia namna nzuri ya kuviendeleza kwa kufuata selebasi maalumu za fani hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: