Baada ya mafanikio ya kongamano la kwanza: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kongamano la pili la (Multaqa Alqamaru Thaqaafi) lenye washiriki (150)…

Maoni katika picha
Kutokana na mafanikio yaliyo patikana katika kongamano la kwanza la (Multaqa Alqamaru Thaqafi) lililo fanywa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, yamepelekea kufanyika kwa kongamano la pili, lenye washiriki (150) kutoka mkoa wa Baabil, ambao ni wanafunzi wa vyuo walimu na watu kutoka katika makundi mengine, kongamano hili linafanyika ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Ameed, kilichopo katika barabara ya Najafu – Karbala, imeandaliwa ratiba kamili inayo endana na viwango vya washiriki, na itakayo wasaidia waweze kupambana na changamoto za kidini, kiutamaduni na kijamii na kuwa mchango mkubwa katika kutatua changamoto hizo.

Ustadh Ali Badri mmoja wa wasimamizi wa kongamano hili ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kongamano hili linamihadhara ya Aqida na mambo mbalimbali ya utamaduni pamaja na mambo ya kutengeneza nafsi na kuandaa viongozi, pia kuna mihadhara inayo baini upotoshaji unao fanywa na vyombo vya habari, na kuonyesha taasisi na vyombo hivyo vinavyo danganya watu, mada zote zinawasilishwa na mashekhe walio bobea na wenye uwezo mkubwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mada hizi ziliteuliwa na jopo la watalamu wanao jua mazingira halisi ya maisha ya wairaq wa leo, kwa hiyo mada hizo zinalenga kutatua changamoto halisi zilizopo katika jamii ya leo na kutoa majibu ya maswali mengi wanayo jiuliza vijana”.

Akaongeza kua: “Sisi tunaamini kuwa vita ya kiutamaduni ipo na inaendelea kuwatafuna wananchi wa Iraq na waislamu kwa ujumla ili kuwatoa katika dini yao na utambulisho wa kitaifa, na kumfanya mtu asiwe na mchango katika jamii na awe hajali yanayo fanyika na aishie kukata tamaa katika kila kitu, jambo hilo kwa sasa ni kubwa katika tabaka la vijana, hivyo ni jukumu letu kurekebisha utamaduni wa ndani na kusambaza upendo na mshikamano na kupinga khitilafu zinazo wanufaisha maadui wa Iraq”.

Kumbuka kua kongamano hili litadumu kwa muda wa siku kumi, katika sehemu yake ya kwanza imehusisha mkoa wa Dhiqaar, tunatarajia kuhusisha mikoa mingine baada ya mkoa wa Baabil, ushiriki katika kongamano hili ni wa hiyari, baada ya kujaza fomu maalumu inayo bainisha lengo la kongamano, Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kuandaa ratiba na wahadhiri inagharamia usafiri, malazi na chakula pamoja na mambo mengine, sehemu ya kwanza ilipata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa washiriki na ilifikia malengo waliyo jiwekea wasimamizi wa kongamano jambo lililopelekea kuanzishwa kwa sehemu ya pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: