Madrasa ya Fatuma bint Asad (a.s) yaendesha semina ya Qur’an kwa wasichana katika majira ya joto...

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati mbalimbali zinazo fanywa na idara za shule za Alkafeel za wasichana zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zinazo fuata selebasi yake ya Qur’an, Madrasa ya Fatuma bint Asad (a.s) imeandaa semina ya Qur’an kwa wasichana wenye umri wa miaka (12) na kuendelea, chini ya mfumo maalumu ulio andaliwa na kamati ya wataalamu, unao endana na umri wa walengwa, nayo inaingia katika semina za majira ya joto zinazo lenga kutumia vizuri kipindi hiki cha likizo za kiangazi, kwa kusoma Qur’an na kuwafanya waipende na kuiingiza katika nafsi zao, kwa ajili ya kutengeneza kizazi cha wasichana wanao jua Qur’an na wenye uwezo wa kupambana na changamoto za maisha kwa kutumia siraha ya Qur’an tukufu.

Semina inafanyika katika kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kilichopo katika mkoa mtukufu wa Karbala, inaratiba kamili ya masomo yafuatayo: (Usomaji sahihi, Hukumuza usomaji, Kuhifadhi Qur’an tukufu) pamoja na vipindi vya tafsiri za baadhi za aya tukufu, inasimamiwa na msomi aliye bobea na mwenye uzowefu mkubwa katika semina za aina hii kwa ajili ya kuhakikisha yanapatikana mafanikio bora zaidi.

Idara ya shule za Alkafeel za wasichana imeandaa usafiri wa washiriki na ulezi wa watoto (wa washiriki) wenye umri wa (mwaka mmoja hadi miaka mitano) bure.

Kumbuka kua kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) ni moja ya vituo vya malezi ya wasichana vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kina idadi kubwa ya shule za dini za wasichana, na hufanya semina za aina mbalimbali kila mwaka zinazo enda sambamba na mfumo wa masomo ya dini yanayo fundishwa shuleni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: