Idara ya umeme ya Atabatu Abbasiyya tukufu: Yatoa huduma daima kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa idara zinazo fanya kazi muda wote katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni idara ya umeme, ambayo ipo chini ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi, inajukumu la kusanifu na kuweka umeme katika miradi mipya inayo tekelezwa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuboresha mitandao ya umeme ndani ya haram tukufu na katika uwanja wa haram pamoja na maeneo yanayo zunguka Ataba, wanasanifu na kuweka njia za umeme chini ya mafungi walio bobea katika fani hiyo pamoja na kuweka ulinzi wa kielektronik, vilevile wanatengeneza vifaa vyote vya umeme katika Ataba tukufu, na wanaunganisha mtandao wa umeme na mitambo ya kufua umeme, wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu wanafunga umeme hadi katika vikundi vya Husseiniyya vinavyo izunguka Ataba na vilivyo karibu yake kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru.

Kwa ajili ya kufahamu zaidi kazi zinazo fanywa na idara hii, tumekutana na kiongizi wa idara Muhandisi Ali Abdulhussein Abbasi ambaye amesema kua: “Idara ya umeme inachukuliwa kuwa moja ya idara muhimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi zake zimegawika sehemu mbili: kwanza, ni kusanifu na kupangilia kila mradi. Pili, ni kusimamia utengaji wa vifaa vyote vinavyo tumia umeme ndani Ataba tukufu, kazi hizo zimegawanywa katika ofisi za idara kama ifuatavyo:

Kwanza: Ofisi ya kukagua umeme, inavifaa maalumu vya kukagulia umeme ndani ya haram na katika uwanja mtukufu wa haram pamoja na maeneo yote yaliyo panuliwa na maeneo ya nje, ofisi hiyo inakituo ndani ya idara, pia ofisi hiyo hutengeneza mabango ya ukaguzi, pia inatengeneza vifaa vya kuzuia majanga ya umeme, aidha wanatumia kifaa cha (3ph) kinacho fanya kazi kwa mizunguko mitatu ya kutengeneza mtambo wa kuwasha taa wakati wa usiku (potoseel).

Pili: Ofisi ya umeme, inajukumu la kufunga mitambo ya umeme pamoja na kuitengeneza, na kufunga feni katika ofisi za vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu sambamba na kuendelea kukagua taa za umeme, hadi katika maeneo ya nje yaliyopo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, fahamu kua vifaa vya mwanzo vinavyo tumika vimetendenezwa Iran na vina ubora wa hali ya juu.

Tatu: Ofisi ya uangalizi wa haram, inajukumu ka kusimamia kazi zote za umeme mpya au za matengenezo zinazo fanywa ndani ya haram tukufu, ikiwa ni pamoja na mataa.

Nne: Ofisi ya uangalizi wa uwanja wa haram, inajukumu la kusimamia umeme katika vitengo vyote vya Ataba tukufu ndani na nje, ndio wenyejukumu la kuwasha taa, kubadilisha rangi za taa na kuwasha taa za mapambo katika siku za mazazi (wilada).

Tano: Ofisi ya winchi, ofisi hii inamiliki winchi nne za umeme kwa ajili ya kazi za idara, pia zinatumiwa na kila kitengo kitakacho zihitaji, kwa mfano: kitengo cha habari na utamaduni huzihitaji kwa ajili ya kupigia picha, kitengo cha usimamizi wa haram huzihitaji kwa ajili ya kazi za usafi, vilevile kitengo cha utumishi hizihitaji kwa ajili ya kazi ya kuweka mapambo, ofisi hii pia inajukumu la kupangilia taa ndani ya uwanja wa haram tukufu.

Sita: Ofisi ya kufunga umeme, inajukumu la kufunga umeme ndani na nje ya uwanja wa haram tukufu, pamoja na kurudia kufunga umeme katika njia za zamani, sawa sawa iwe ndani ya haram au katika maeneo yaliyo ongezwa na Ataba tukufu hivi karibuni.

Saba: Ofisi ya kusimamia utendaji wa ngazi (lifti) za umeme, Ofisi hii inajukumu la kusimamia na kukagua utendaji wa ngazi (lifti) zote za umeme zilizopo katika vitengo vyote vya Ataba tukufu, pamoja na maeneo ya nje yaliyopo chini ya Ataba, na hugawa majukumu maalumu kwa vitengo vingine.

Kumbuka kua idara hii ni sawa na idara zingine za kitengo cha uangalizi wa kihandisi, inaendeshwa na watalamu walio bobea katika kazi zao wenye uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yao ya kiufundi, idara hii inamchango mkubwa katika kuhakikisha inajitegemea katika utendaji wa kazi zake, kwa ajili ya manufaa ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na haitegemei msaada wowote kutoka nje kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: