Hospitali ya rufaa Alkafeel yagharamia uwekaji wa viungo bandia kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi…

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imegharamia uwekaji wa viungo bandia kupitia kituo cha Abulfadhil Abbasi (a.s), miongoni mwa misaada ya kibinadamu wanayo toa ni uwekaji wa viungo bandia kwa majeruhi wa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, walio poteza viungo katika uwanja wa utukufu, kama sehemu ya kuonyesha kuwajali kwa namna walivyo jitolea kwa ajili ya kukomboa taifa na maeneo matukufu.

Viungo bandia hivyo; kwa mujibu wa maelezo ya mtalamu wa majeraha ya kuvunjika viungo katika hospitali hiyo, Dokta Usama Abdulhussein: “Vilikua vya aina mbili: kuna viungo tambuzi na viungo vya kawaida, viungo hivyo vina uwezo mkubwa, vitawasaidia majeruhi waweza kutembea kawaika, na kuwa mbadala wa viungo walivyo poteza na vitawapa matumaini mapya”.

Akafafanua kua: “Aina hii ya viungo, huchukua saa mbili kuvifunga kwa mgonjwa, na maada ya hapo anaweza kusimama na kutembea kama kawaida, inatofautiana na aina ya zamani ambayo ilikua inachukua hadi siku tatu katika ufungwaji wake kwa mgonjwa, majeruhi walio wekewa viungo bandia wanatoka mikoa tofauti na katika vikosi tofauti vya Hashdi Sha’abi, walitibiwa katika Hospitali ya Alkafeel siku za nyuma bila malipo pia”.

Kumbuka kua Hospitali ya rufaa Alkafeel tangu ilipo tolewa fatwa tukufu ya kujilinda, kama zilivyo taasisi zingine za Atabatu Abbasiyya tukufu, imechukua majukumu ya kuwatibu wapiganaji wanao jeruhiwa vitani na kufanya kila iwezalo kwa ajili ya kuwapunguzia machungu yao, jambo hilo ni utekelezaji wa agizo la Marjaa dini mkuu, pia ni sehemu ya kutekeleza wajibu wake kwa majeruhi, sambamba na kuwatibu pia hubeba jukumu la kuwapa viungo bandia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: