Kwa picha: Kuanza kwa kazi ya kusafisha kubba na minara miwili ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wameanza kazi ya kusafisha kubba na minara miwili ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo huifanya kwa vipindi maalumu kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo husababisha kuathirika kwa kubba na minara hiyo, kutokana na kujaa vumbi katika vifuniko vya dhahabu, husafishwa kwa mfumo wa duara ambao husaidia kuimarisha zaidi vifuniko hivyo na kuvifanya visiharibike.

Kazi hii inafanywa kwa kufuata utaratibu maalumu na kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo haviathiri vifuniko vya dhahabu vilivyopo katika kubba na minara, pamoja na kuzingatia mazingira ya hali ya hewa na kwa umakini mkubwa, hatua ya kwanza inahusisha kusafusha kubba tukufu katika sehemu tano, kila siku inasafishwa sehemu moja, walianza kusafisha upande wa mashariki mkabala na mlango wa Furaat (Alqami) na upande wa saa kwa kuanzia juu kuja chini, ambao ni upande wa bendera tukufu hadi katika kitako cha kubba, baada ya kumaliza kusafisha kubba ndio wataanza kusafisha minara kwa mfumo tofauti na huu wa kusafisha kubba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: