Maahadi ya Qur’an tukufu ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya yakatusha taarifa zilizo sambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuhusu kushirikiana kwake na vyombo vya habari nje ya Ataba tukufu…

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’an tukufu chini ya Maahadi ya Qur’a ya Atabatu Abbasiyya kimekanusha taarifa zilizo sambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii, ya kuwepo kwa ushirikiano au makubaliano yeyote na taasisi yeyote ya habari nje ya Ataba tukufu kwa ajili ya kufanya mashindano ya Qur’an chini ya mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa au mradi mwingine wowote.

Kituo kimeongeza kua: Hakuna makubaliano kama hayo, jambo hilo sio sahihi kabisa, tambua kua mradi wa kiongozi wa wasomaji una utaratibu maalumu, ulianzishwa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu na una wasimamizi kamili.

Kumbuka kua mradi wa kiongozi wa wasomaji, ni miongoni mwa miradi bora ya Qur’an tukufu ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya, na hufanywa chini ya walimu wenye uwezo mkubwa kutoka ndani na nje ya Iraq, unalenga kutengeneza kizazi cha wasomi wa Qur’an na kulea vipaji vya watoto katika usomaji wa Qur’an ndani ya muda mfupi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: