Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya semina kwa watumishi wake…

Maoni katika picha
Miongoni mwa semina zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa watumishi wake, na kuchangia kuongeza ujuzi wao katika kupambana na majanga yanayo weza kutokea kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni semina hii iliyo fanyika hivi karibuni.

Kwa maelezo zaidi kuhusu semina hiyo tumeongea na msimamizi wa semina Ustadh Bilali Jabbaar Jaasim ambaye pia ni kiongozi wa madaktari wa dharura, amebainisha kua: “Kufuatia maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu kuhusu umuhimu wa kufanya semina za kufundisha namna ya kupambana na majanga ya kimaumbile, kama vile matetemeko, vimbunga pamoja na majanga ya kibinadamu, kama vile moto, matukio ya kigaidi na mengineyo, na namna ya kupambana na kutatua matatizo hayo ndio tumefanya semina hii”.

Akaongeza kua: “Kutakua na semina nne za aina hii ambazo watashiriki watumishi wa vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na jopo la wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), kila semina itachukua siku mbili na kila siku itakua na saa tano za masomo, semina zitakua na masomo ya vitendo pia, siku ya mwisho kutakua na maonyesho ya vitendo kuhusu namna ya kuonkoa nyumba au majengo”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Kupitia semina hizi zitasaidia kuandaa kikosi kamili ndani ya vitengo vya Ataba chenye jukumu la kupambana na majanga ya kimaumbile na kibinadamu na kuokoa uhai wa watu kwa kutumia mbinu sahihi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: