Kamati ya maelekezo na misaada ya Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa misaada kwa wapiganaji waliopo mpakani na Siriya…

Maoni katika picha
Bado kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendelea kuwatembelea na kutoa misaada kwa wapiganaji na Hashdi Sha’abi, pamoja na kuisha kwa vita na kukombolewa ardhi yote ya Iraq, safari hii wametembelea wapiganaji walio itikia fatwa ya Marjaa dini mkuu waliopo katika mpaka wa Iraq na Siriya pamoja na baadhi ya vikosi vilivyopo katika wilaya ya Sanjaar.

Ni sehemu ya muendelezo wa misafara ya kusaidia inayo fanywa na kamati hii toka ilipo tolewa fatwa tukufu na Marjaa dini mkuu ya jihadi ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu, ziara hii imehusisha vikosi vyote, vya jeshi la serikali, polisi na Hashdi Sha’abi.

Kiongozi wa kamati na rais wa ujumbe huo Shekh Haidari A’aridhi ameongea kuhusu msafara huu kua: “Kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu ya kuwasaidia wapiganaji, ujumbe wa kamati ya maelekezo na misaada chini ya kitengo cha dini imewatembelea wapiganaji waliopo katika mpaka wa Iraq na Siriya, na kuwapa misaada ya baadhi ya vitu muhimu kwao pamoja na baadhi za zawadi za tabaruku kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambazo huwajenga kiimani, tumetembelea vikosi mbalimbali vya Hashdi Sha’abi vinavyo linda amani katika eneo hili la mpakani, ziara yetu imechukua siku tatu na tumetembea eneo la kilometa (120) tumefanikiwa kutembelea wapiganaji wote waliopo katika eneo hilo”.

Akaongeza kua: “Tuliwakuta wapiganaji wakiwa na hamasa kubwa pamoja na ugumu wa mazingira ya hali ya hewa na uchache wa vifaa, hakika wamejitolea nafsi zao kwa ajili ya kuhakikisha magaidi hawakanyagi tena katika ardhi ya Iraq, baada ya kukomboa ardhi ya Iraq kutokana na utukufu wa ndugu zao, na wao leo wamekua ngome imara dhidi ya kila atakaye taka kuharibu amani na utulivu wa taifa hili”.

Wapiganaji wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwa pamoja nao katika uwanja wa vita na katika maeneo yaliyo kombolewa, wakasisitiza kua jambo hili linawapa moyo zaidi wa kuendelea kuwa ngome imara dhidi ya kila atakaye taka kuharibu amani na utulivu wa taifa hili.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hutuma misafara ya kwenda kutoa misaada ya vyakula na vifaa kwa vikosi vya wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abi, pamoja na kuunda kamati maalumu ya kusaidia familia za mashahidi na kufuatilia hali za majeruhi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: