Kongamano la awamu ya pili la Multaqa Alqamaru Thaqafi lapata matokeo mazuri…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza siku tano za kongamano la kitamaduni, na kutokana na mada mbalimbali zilizo wasilishwa katika kongamano hilo linalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, limepata matokeo mazuri kwa washiriki wake wapatao (150) kutoka katika mkoa wa Baabil, jambo hilo limetokana na uzuri wa ratiba iliyojaa vipengele vingi, pamoja na ubora wa uwasilishaji unao endana na mazingira halisi ya changamoto zilizopo katika jamii.

Mtandao wa Alkafeel haukubaki nyuma, umefanya mahojiano na washiriki ambao kila mmoja ametoa maoni yake, bwana Muyassir Abbasi Juburi Mhitimu wa chuo kitivo cha malezi kitengo cha michezo amesema kua: “Kutokana na ushiriki wangu katika kongamano hili nimefaidika sana na nimeongeza elimu, hususan katika nyanja ya habari, na namna ya kuzifanyia kazi habari za upotoshwaji na kusoma kilicho andikwa na kuweza kubaini kama ni sahihi au sio sahihi, hakika warsha hii imekuja kutatua matatizo halisi yaliyopo katika jamii, tunawashukuru sana wasimamizi wa kongamano hili pamoja na wakufunzi walio tufundisha kwa ustadi mkubwa na kwa kutumia mifano halisi iliyo tufanya tuelewe kwa urahisi, nikipata nafasi nyingine nitashiriki tena kwa kishindo”.

Naye bwana Husaam Aadil Muhammad mwanachuo wa kitengo cha kemiya amesema kua: “Kongamano hili limeandaliwa kwa ajili ya kuongeza maarifa ya kiutamaduni, kidini, kifikra na kijamii kutokana na mada tulizo fundishwa, ambazo zinagusa kila nyanja ya maisha yetu, zina mjenga mtu, kukuza elimu, kutoa utata, kufichua habari zisizo sahihi na kutambua njia zinazo tumiwa na vyombo vya habari katika kupotosha habari nk.., tumefundishwa kwa njia nzuri na rahisi kuelewa inayo endana na viwango vyetu, mada zote tulizo fundishwa zinaendana na mazingira yetu halisi, hakika zitasaidia sana kutatua changamoto za kijamii, kifikra na kiutamaduni kwa vijana”.

Bwana Ahmad Mahmuud Hassan mhitimu wa digrii ya malezi na michezo amebainisha kua: “Amepata alicho kua anatarajia wakati alipo ingia katika kongamano hili, ameweza kubadilisha fikra zake, na sasa anaweza kutafakari kwa makini na kubaini mambo mazuri katika uhai wake kielimu, akasema: nitakua balozi wa yote niliyo soma hapa kila mahala nitakapo kwenda”.

Bwana Hassan Ali Quraishi akaongeza kua: “Nimefaidika sana kutokana na mada za utamaduni, aqida na za habari zilizo wasilishwa, zilichanganyika baina ya ugumu baadhi ya muda na wepesi, nimezipenda sana mada zilizo wasilishwa na wala hazikunichosha, naamini kongamano hili litasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamato katika jamii kama washiriki watayafanyia kazi mambo waliyo soma katika miji yao”.

Naye bwana Alaa Haadi Abbasi mwanafunzi wa sekondari ameonyesha furaha ya kushiriki kwake kwa kusema kua: “Nina bahati sana kukutana na walimu wenye uwezo mkubwa pia nimepata fursa ya kujuana na washiriki wa kongamano kutoka katika mkoa wa Baabil, jambo zuri zaidi, kongamano hili limekusanya elimu zote na fikra tofauti, pia linaongeza elimu na kujiamini sambamba na kuvunja uoga na hofu, jambo hilo ni tatizo kubwa kwa vijana katika mitihani yao na masomo kwa ujumla, mada zimewasilishwa kwa njia rahisi na yenye kueleweka vizuri, kwa hakika utukufu wote uwaendee walimu walio fanya juhudi kubwa ya kutufikishia elimu”.

Bwana Ahmad Muhammad Ali Mhitimu wa Maahadi ya ufundi amesisitiza kua “Hakika mambo yote yaliyo someshwa katika kongamano hili ni mambo halisi, yana faida kubwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tunatarajia yawe chahu ya kutatua changamoto tulizo nazo, tunawapongeza sana wasimamizi wa kongamano hili na tunaomba yandelee kufanyika makongamano ya aina hii kwa hakika muda si mrefu tutaona matunda yake”.

Kumbuka kua kongamano hili linafanyika kwa muda wa siku kumi, hatua ya kwanza ilihusisha watu wa mkoa wa Dhi Qaar, tunatarajia kuhusisha mikoa mingine baada ya mkoa wa Baabil, ushiriki katika kongamono hili ni kwa hiyari baada ya kujaza fomu inayo bainisha malengo ya kongamano, Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kuandaa ratiba na wahadhiri, inagaramia pia usafiri, malazi na chakula pamoja na mambo mengine, kongamano la kwanza lilikua na mwitikio mkubwa kutoka kwa washiriki na lilifikia malengo yake ndio ikawa sababu ya kuandaa kongamano la pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: