Baada ya serikali kushindwa kuwatimizia: Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua kituo cha afya katika kijiji cha Aali Malaal…

Sehemu ya uwekaji wa vifaa vya kituo cha afya
Miongoni mwa matukio ya kibinadamu, Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua kituo cha afya katika kijiji cha Aali Malaal mkoani Dhi Qaar, kipo baina ya kituo cha polisi cha wilaya upande wa kaskazini na kitongoji cha Nnasru, nacho ni miongoni mwa mamia ya vijiji ambavyo vimesahauliwa na serikali kwa kiasi kikubwa kuwekewa huduma za kibinadamu, wakazi wa kijiji hicho wana maisha magumu na wanaupungufu mkubwa wa chakula na huduma za kijamii, pai kuna maradhi ya mripuko katika kijiji hicho chenye kaya (30) na watu wanao kadiriwa kufika (650) walikua hawana kituo cha afya, na ilikua vigumu kupeleka wagonjwa wao katika vituo vilivyopo katika miji ya jirani jambo hilo halikidhi matakwa ya kitabibu.

Waliendelea kuhangaika na hali hiyo hadi kilio chao kilipo fika kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kunyoosha mikono yake kuwaokoa katika mazingira magumu waliyo nayo, kwa kuwajengea kituo cha afya na kukiita (Nyumba ya afya katika kijiji cha Aali Malaal), baada ya wakazi wa kijiji hicho kujitolea ardhi ya kujenga kituo hicho, hakika kituo hiki kimejengwa, pamoja na serikali kushindwa kuwatekelezea jambo hilo, na kimekabidhiwa ofisi ya afya ya mkoa wa Dhi Qaar kwa ajili ya kuweka madaktari na wauguzi.

Atabatu Abbasiyya tukufu imetuma ugeni rasmi ukiongozwa na rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhi Ni’mah Salmaan kwa ajili ya kuzindua kituo hicho na kuweka vifaa, naye ametuambia kua: “Ujenzi wa kituo hiki ulianza baada ya kufikiwa na maombo ya wakazi wa kijiji hiki kupitia wawakilishi wao, maombi yao yalipo fikishwa kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aliidhinisha ujenzi wa kituo hiki pamoja na kuweka vifaa muhimu likiwemo jenereta la kufua umeme”.

Akaongeza kua: “Hakika kituo hiki pamoja na udogo wa jengo lake lakini kitatoa huduma kubwa na kumaliza tatizo la muda mrefu la wakazi wa Aali Malaal, hasa baada ya serikali kushindwa kuwatekelezea jambo hili kwa miaka mingi”.

Watu wa Aali Malaal wameonyesha shukran zao za dhati kwa kujengewa kituo hiki ambacho serikali imeshindwa kuwajengea kwa miaka mingi, wakitarajia kianze kufanya kazi ndani ya muda mfupi.

Kumbuka kua kazi hii ya kibinadamu ilitanguliwa na kazi nyingine ambayo ni ujenzi wa kituo kamili cha kusafisha maji yanayo tosheleza wakazi wa kijiji hicho, baada ya kubaini tatizo la maji safi ya kunywa walilo kuwa nalo na lililo kua likiwasababishia mripuko wa magonjwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: