Daru Rasuul A’adham (s.a.w.w) ipo katika maandalizi ya mwisho ya kongamano la kimataifa la kwanza…

Maoni katika picha
Daru Rasuul A’adham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya maandalizi ya mwisho ya kongamano la kimataifa la kwanza, litakalo fanyika (3-4 Dhul-Hijja 1439h) sawa na (16-17 Agosti 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu anaye wasomea kurasa zilizo takasifu), na anuani isemayo: (Mwenendo wa Mtume ni sheria ya Mola katika maelekezo ya kibinadamu), kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Aadil Nadhiir.

Akaongeza kua: “Kongamano hili la kimataifa linachukuliwa kuwa miongoni mwa makongamano muhimu yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, tumeandaa vitu vingi kwa ajili ya kuhakikisha linakua kongamano bora, tumefanya vikao vingi vya maandalizi, miongoni mwa vikao hivyo ni kikao hiki cha mwisho ambacho tumepitisha vipengele vya mwisho vya kongamano hilo”.

Akabainisha kua: “Katika kikao hiki tumejadili mambo mengi yanayo husiana na ratiba, jambo kubwa zaidi lilikua ni kuweka ratiba ya kufunga kongamano, ambapo kutakuwa na uwasilishwaji wa mada za kitafiti, pamoja na kuandaa mialiko ya washiriki”.

Kumbuka kua kongamano hili la kielimu linalo elezea historia ya Mtume Mtumufu (s.a.w.w) ni la kwanza, nalo ni muendelezo wa mazowea ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuonyesha umuhimu wa elimu katika nyanja mbalimbali, kwa kufanya makongamano ya kielimu yanayo endana na maendeleo ya sasa, tunataka akili za watafiti zizame katika kuchambua historia ya Mtume, na tupate mambo ya uhakika katika historia yake tukufu tutakayo weza kuyapata, historia yake ina muelekeo wa kifikra wa pekee tofauti na mielekeo ya kifikra na kijamii mingene, ina athari kubwa katika maswala ya sheria za kiislamu na inaendana na mielekeo ya Qur’an tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: