Uongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji umetangaza kutokea mripuko katika hifadhi ndogo ya siraha za kikosi hicho iliyopo katika mji wa Alwand umbali wa kilo meta (20) kaskazini ya mkoa wa Karbala, taarifa zinasema kua mripuko huo umesababishwa na kuongezeka kiwango cha joto.
Uongozi wa kikosi ukaongeza kua: “Imetolewa amri ya kufanya uchunguzi wa haraka kuhusu tukio hilo, ushahidi wa awali hauonyeshi kama mribuko huo umesababishwa na uharibifu” inaonyesha kua: “Hasara iliyo patikana ni ya vifaa peke yake hakuna maafa ya kibinadamu”.
Taafira yenye nguvu inasema mripuko umesababishwa na ongezeko la joto.