Siku ya kutandikwa ardhi…

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi ishirini na tano Dhulqa’ada ni usiku wa kutandikwa ardhi –kutandikwa ardhi chini ya Alkaaba juu ya maji- ni usiku mtukufu sana hushuka rehma za Mwenyezi Mungu mtukufu katika usiku huo, kufanya ibada ndani ya usiku huo kuna malipo makubwa.

Na mchana wa mwezi ishirini na tano ni siku ya kutandikwa ardhi: nayo ni moja ya siku nne ambazo zimesuniwa kufungwa ndani ya mwaka, imepokewa kuwa: kufunga katika siku hizo ni sawa na kufunga miaka sabini, na nikafara ya dhambi za miaka sabini, katika riwaya nyingine, atakaye funga siku hii na akaswali swala za usiku ataandikiwa thawabu sawa na mtu aliye fanya ibada miaka mia moja, na ataombewa msamaha na kila kitu kilichopo baina ya mbingu na ardhi, ni siku ambayo rehma ya Mwenyezi Mungu mtukufu huwaenea waja wake, kufanya ibada na kumtaja Mwenyezi Mungu katika siku hiyo kuna thawabu nyingi sana.

Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (je! Vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga * Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. * Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. * Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi) maana ya neno “Dahwu” ambalo linasema “Dahaaha” ni, akaitandika na akainyoosha, akaifanya kuwa mahala pazuri pa kuishi, Shekh Muhammad Jawaad Mughniyya amesema katika tafsiri Alkashaafu kua: Aliitandika na kuiandaa ikawa mahala pazuri kwa kuishi na kutembea, na katika kitabu cha (Kufahamu zama za Qur’an) neno: “Dahaaha” amelitafsiri kua, ameifanya ardhi kama yai, tafsiri hiyo inakubaliana na watalamu wa falaki kua ardhi ipo kama yai… na nezo “Daha” linamaanisha pia kutandika, ni neno pekee la kiarabu ambalo linamaanisha kutandika na kunyoosha kwa wakati mmoja, kwa hiyo inamaanisha kua ardhi ameitandika na akaiweka katika umbo la yai, (la duara), pia inaonyesha upeo wa hali ya juu katika lugha na uwezo wa kuchagua maneno yenye maana ya ndani.

Kutoka kwa Imamu Ali Kiongozi wa waumini (a.s) anasema: (Hakika rehma ya kwanza ilishuka ardhini kutoka mbinguni katika siku ya ishirini na tano ya mwezi wa Dhulqa’ada, atakaye funga siku hiyo na akaswali swala za usiku ataandikiwa ibada za miaka mia moja, sawa na kafunga na kuswali miaka mia moja, watu wowote watakao kusanyika siku hiyo na wakamuomba Mwenyezi Mungu haja zao hawata achana hadi Mwenyezi Mungu atakuwa amewakidhia haja zao, katika siku hiyo hushuka rehma milioni moja, rehma tisini na tisa huwa ni maalumu kwa ajili ya watu walio funga na kuswali katika usiku huo).

Sehemu ya kwanza iliyo ainishwa katika ardhi hii ni sehemu ilipo Alkaaba tukufu, kisha Mwenyezi Mungu mtukufu akatangika ardhi kutokea sehemu hiyo, sehemu hiyo ndio kitovu ambapo ardhi yote imetandikwa kutokea hapo, ndio maana ya kutandikwa ardhi kutokea chini ya Alkaaba tukufu, unaweza kuhakikisha hilo kutokana na baadhi za riwaya zilizo pokelewa na Ahlulbait (a.s) imepokewa kutoka kwao (a.s) kua: ardhi ilitandikwa baada ya miaka elfu mbili tangu kuumbwa kwake.

Imepokewa katika kitabu cha Mafaatihu Jinaani cha Shekh Abbasi Qummi, Siku hii pamoja na kufunga na ibada za kumtaja Mwenyezi Mungu mtukufu kuna ibada zingine nyingi, miongoni mwake ni: Swala ya rakaa mbili ambayo utaiswali wakati wa Dhuha, utasoma Alhamdu mara moja na surat Shamsi mara tano katika kila rakaa, baada ya salamu useme: (Laa haula wa laa quwata illaa billahil aliyyil adhiim) kisha usome dua hii: (Yaa muqiila atharaati aqilnii athratii, yaa mujiiba da’awaati ajib da’awatii, yaa saami’al aswaati isma’a swautii, warhamnii, wa tajaawaz an sayyiaatii wa maa indii yaa dhaljalaali wal ikraam).

Fahamu kua siku ya kutandikwa ardhi (Dahwul ardhi) ni siku ya kesho Juma Tano kwa mujibu wa kalenda ya Hijiriyya (25 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (8 Agosti 2018m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: