Hakika kulea watoto katika mazingira ya Qur’an kunasaidia kutengeneza kizazi chenye kushikamana na dini, na kunawasaidia kufahamu mafundisho ya dini ya kiislamu mapema katika uhai wao, Qur’an tukufu ni burudisho la nafsi, inapo somwa roho huchanua na hunawirika kwa maneno ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Kwa lengo la kuingiza Qur’an katika roho za vijana wa baadae na katika mahudhurio makubwa, bado semina za majira ya kiangazi za kufundisha usomaji wa Qur’an tukufu na kuihifadhi kwa wanafunzi zaidi ya elfu kumi na nane zinaendelea katika sehemu mbalimbali na kwenye mikoa tofauti hapa Iraq, zinazo simamiwa na Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na wanafunzi elfu mbili walio gawanywa katika halaqa (vikundi) vinavyo itwa Rasuul Al-Akram (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watoharifu (a.s), semina hizi zinahusisha masomo kadhaa: usomaji wa Qur’an tukufu na masomo ya Fiqhi na Aqida, yanayo fundishwa na walimu walio bobea wenye uzowefu wa zaidi ya miaka arubaini na tano, kila siku wanasoma kwa muda wa saa tatu, mazingira ni mazuri ya kiimani yamepambwa na maneno ya Mwenyezi Mungu na historia ya Mtume wake mtukufu na watu wa nyumbani kwake watakatifu.
Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawadi Nasrawi amebainisha kua: “Hakika viwango vya wanafunzi na mafanikio yaliyo patikana ndani ya muda huu mfupi yanatufurahisha, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tumefanikiwa kufundisha zaidi ya wanafunzi (18000) masomo mbalimbali yaliyo wapa msimamo na mwongozo katika maisha yao”.
Kumbuka kua mradi huu unalenga kutengeneza kizazi kitakacho ishi kwa mujibu wa vizito viwili –Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu- idadi wa washiriki inaendelea kuongezeka mwaka baada ya mwaka, mradi huu ulianza na wanafunzi (150) mwaka 2011 kisha wakaongezeka hadi zaidi ya wanafunzi (6000) mwaka 2014 na katika mwaka wa 2016 wakawa zaidi ya (10,000) wakaendelea kuongezeka hadi mwaka 2017 wakawa zaidi ya (16000).