Mito ya kupanua wigo yatolewa katika hitimisho la kongamano la kitamaduni Multaqal-Qamaru awamu ya pili…

Maoni katika picha
Alasiri ya Juma Nne (24 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (7 Agosti 2018m) lilihitimiswa kongamano la kitamaduni Multaqal-Qamaru awamu ya pili, ambalo ni kongamano la kitamaduni, kimwongozo na kukuza uwezo, linalenga kuongeza uwezo wa uwelewa wa kitamatuni na kimazingira kwa raia wa Iraq, kongamano hili husimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na lilikua na washiriki zaidi ya (150) kutoka katika mkoa wa Baabil, watu wa tabaka tofauti, wasomi wa sekula, watu wa malezi na wanafunzi wa masomo ya dini, yote yamefanyika kwa kuwasiliana na mawakili wa Marjaa dini wa mkoa huo.

Hafla ya kufunga kongamano hilo ilifanyika ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Ameed, baada ya kusoma Qur’an ya ufunguzi wa hafla na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ulifuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na mjumbe kutoka katika kitengo cha dini Sayyid Muhammad Mussawi, alianza kwa kuwasalimia washiriki wa kongamano hili, akaeliza matumaini yake watakua wamenufaika kwa kiasi ambacho watachangia kutengeneza kizazi chema, akawataka kunufaika na harakati za maelewano na wazisome kwa umakini na kuziiga, miongoni mwa harakati hizo ni harakati za Mtume mtukufu Muhammad (s.a.w.w) na mjukuu wake Imamu Hussein (a.s), akabainisha kua: “Hakika miongoni mwa sababu za kufanikiwa kwa harakati yeyote njema ni kushikamana kwao na Mwenyezi Mungu mtukufu, ili naye adumishe rehema zake kwao, pia wanatakiwa kuwa na tabia njema sambamba na kuendelea kujielimisha na kuwa na utamaduni mzuri, vitu hivyo ndio siraha yao dhidi ya kila atakae wapinga na kuwapiga vita katika uhai wao”.

Ukafuata ujumbe wa waandalizi wa kongamano hili –kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu- ambao uliwasilishwa na naibu rais wa kitengo Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, ambaye alibainisha kua: “Tunaona fahari kukutana na sura hizi takatifu za waumini kutoka katika mkoa wa Baabil, mkoa wa utukufu na historia, nimatumaini yangu wahadhiri wa kongamano hili wamekupeni elimu kubwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu itakua mbegu nzuri ya kupata viongozi wema katika jamii, tunategemea muwe msaada mkubwa katika kupambana na changamoto mbalimbali zinazo ikumba jamii, bila kusahau changamoto za kifikra na kiitikadi”.

Akabainisha kua: “Hakika watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa mazuwaru, wigo wa huduma unapanuka na kujumuisha vitu vingi, hawaishii katika huduma wanazo toa moja kwa moja kwa zaairu, wanavituo na taasisi za kisekula na kitamaduni pamoja na vituo vya utafiti vinavyo fanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kutoa huduma zinazo changia kutengeneza jamii njema”.

Washiriki walitoa tamko la shukrani kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia muwakilishi wao Ustadh Ahmad Naaif, ambaye alibainisha kua: “Hakika kongamano hili la (Multaqal-Qamar) linatokana na Abulfadhil Abbasi (a.s), tumepata faida kubwa kutokana na mihadhara pamoja na masomo yaliyo someshwa, yatatusaidia sana kupambana na changamoto zinazo tuzunguka katika jamii, hususan tabaka la vijana ndio wahanga wakubwa wa changamoto hizo, kila mtu anatakiwa apambane kwa nafasi yake, tunatakiwa tufikishe tulicho jifunza katika kongamano hili kwa watu wengine ambao hawakuweza kushiriki, tunatakiwa tutafsiri kwa vitendo yale tuliyo soma ili matunda yake yaonekane katika jamii, siku hii ya kufunga kongamono sio siku ya mwisho, bali ni siku ya kwanza ya kuyafanyia kazi elimu tuliyo ipata, tunaomba liendelee kufanyika kongamano hili na liwe na uwanja mkubwa zaidi”.

Hafla ilipambwa na visomo vya mashairi pamoja na utowaji zawadi kwa washiriki, na mwisho kabisha washiri wote wa kongamano wakapewa vyeti ya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: