Kituo kimetoa wito kwa wataalamu wote na watafiti waje kushiriki katika kongamano hili muhimu la kielimu na kimataifa.
Mada za kongamano:
Mada ya kwanza: Maandalizi ya kiufundi ya sekula katika sekta ya kupangilia kwa namba na changamoto za mazingira ya namba.
Mada ya pili: Namna na nyenzo za kupangilia maarifa katika mazingira ya namba.
Mada ya tatu: Mpangilio wa vipimo na misingi ya mpangilio wa kisasa.
Mada ya nne: Taasisi za elimu na nafasi zake katika kupangilia maarifa kwa namba.
Masharti ya utafiti:
- - Utafiti uandikwe kwa kiarabu au kiengereza.
- - Usizidi kurasa (25) za (A4).
- - Utumwe kupitia barua pepe katika kamati ya barua na uandikwe katika program ya (word).
- - Mtafiti abainishe mada anayo andika na aambatanishe na wasifu (cv) yake.
- - Utafiti usiwe umesha tolewa katika kongamano au nadwa na watu wengine.
- - Mtafiti azingatie kanuni za kielimu katika uandishi wake.
- - Tafiti zitakazo kidhi vigezo zitaingizwa katika mchujo.
Fahamu kua tarehe ya mwisho ya kupokea mihtasari ni (1/10/2018m) na tarehe ya kujibiwa mihtasari hiyo ni (20/10/2018m), na tarehe ya mwisho ya kupokea tafiti ni (10/12/2018m) na tarehe ya kujibiwa ni (1/1/2019m).
Tafiti zote zitumwe kupitia barua pepe ifuatayo: Info@Lccis.Net au Informatics2019@gmail.com
Kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07712868460 au 07703066696).