Atabatu Abbasiyya tukufu yagawa maelfu ya lita za maji kwa wakazi wa mji mkongwe wa Karbala na makumi ya vipande vya barafu kila siku...

Maoni katika picha
Kutokana na kuongezeka kiwango cha joto pamoja na kuongezeka kwa haja ya maji safi ya kunywa na barafu, kutokana na tatizo la kukatika katika kwa maji na umeme, jambo hili limepelekea idara ya umwagiliaji chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu waongeze juhudi ya kuwapa wakazi wa mji mkongwe wa Karbala na maeneo yanayo zunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kiwango cha maji yanayo sambazwa kwa siku kimefika zaidi ya lita laki saba (700,000) pamoja na makumi ya vipande vya barafu.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Ahmadi Hanuun ameuambia mmtandao wa Alkafeel kua: Mnyeshaji maji; Ni moja ya majina aliyo pewa Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na hilo ni jukumu la idara yetu kuwapa maji bure wakazi wa mji mkongwe wa Karbala pamoja na nyumba zinazo zunguka haram tukufu, tunagawa maji safi ya kunywa pamoja na barafu huduma ambayo inahitajika zaidi na wakazi hao pamoja na mazuwaru kwa sasa kutokana na kuongezeka kiwango cha joto, na tatizo la kukatika katika kwa umeme na maji.

Akaongeza kusema kua: Ugawaji wa maji unafanyika kupitia kituo maalumu kilicho unganishwa na kituo kikuu cha Atabatu Abbasiyya tukufu na maji safi na yenye ubora wa hali ya juu, maji hayo hupozwa kwa viwango vizuri na kutiwa katika mahodhi maalumu kisha huwekwa barafu kutoka katika kiwanda cha barafu cha Ataba tukufu, wakazi huchukua maji kutoka katika maeneo maalumu kwa kiwango wanacho hitaji, na humpa barafu kila anaye hitaji, kazi hii inafanyika muda wote.

Akasisitiza kua: Kila siku kiwango cha maji yanayo sambazwa kinafika lita laki nne na elfu themanini (480,000) na katika baadhi za siku hufika hadi zaidi ya lita laki saba na elfu ishirini (720,000) pamoja na mamia ya vipande vya barafu tunavyo vipata kutoka katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi ya kugawa maji hufanyika wakati wote ndani ya mwaka mzima, lakini mahitaji huongezeka zaidi wakati wa joto, ambapo watumishi wa kitengo hiki huongeza kasi ya ugawaji maji katika haram tukufu na maeneo yanayo izunguka pamoja na kuvipa maji na barafu vikundi vya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: