Idara ya uangalizi wa utendaji wa ngazi na lifti inaendeleza juhudi za matengenezo ya ngazi hizo katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Baada ya kukaribia kumaliza mwaka tangu kuanzishwa kwake mafundi wa idara ya ngazi na lifti chini ya kitengo cha uangalizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata mafanikio makubwa katika utendaji wa majukumu yao kwa kukarabati zaidi ya ngazi (60) za umeme ndani na nje ya Ataba tukufu, pamoja na milango ya umeme iliyopo ndani ya haram tukufu, idara hii imepata mafanikio makubwa katika utendaji wake.

Kiongozi wa idara ya umeme katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi Muhandisi Ali Abdulhussein Abbasi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Idara hii ilianzishwa kutokana na maendeleo ya ujenzi wa kisasa unao fanyika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pia kwa ajili ya kubana matumizi makubwa ya pesa yaliyo kua yakifanyika kwa ajili ya kukarabati ngazi na lifti za Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya muda mfupi mafundi hao wameonyesha mafanikio makubwa katika sekta hiyo, wakati siku za nyuma matengenezo yalihusisha mambo madoqo madogo ya kimakenika peke yake”.

Akaongeza kusema kua: “Kazi zinazo fanywa na idara hii za kukarabati ngazi na lifti zinahusisha kazi za makenika na kazi za umeme, pamoja na kupangilia ngazi, idadi ya ghorofa na kasi ya ngazi, idara ya ngazi imegawanywa sehemu mbili, sehemu ya kukagua ngazi wakati wote na sehemu ya matengenezo”.

Akaendelea kusema: “Kazi za idara hii haziishii kwenye kutengeneza ngazi na lifti peke yake, bali wanatengeneza ngazi za kawaida na ngazi za umeme, pia idara inajukumu la kuandaa vifaa vitakavyo tumika katika ngazi kwa kuwasiliana moja kwa moja na makampuni ya kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha wanapata vifaa bora zaidi ndani ya muda mfupi na kwa gharama nafuu, tofauti na kutumia mawakala katika kufikia makampuni hayo, sambamba na matengenezo ambayo wanafanya wao wenyewe bila kuhitaji msaada wowote wa mafundi kutoka nje, kuna miradi mingi mikubwa na midogo ambayo imekamilika, tena imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na mafundi wa idara ya uangalizi wa utendaji wa ngazi na lifti chini ya idara ya umeme ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: