Hivi punde: Umetokea mripuko katika hifadhi ya siraha za kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, kikosi kinachukulia kua tukio hili ni la kukusudia…

Maoni katika picha
Adhuhuri ya leo Ijumaa (27 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (10 Agosti 2018m) umetokea mripuko katika moja ya hazina za siraha za kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika kitongoji cha Razaza bila kusababisha hasara za kibinadamu.

Viongozi wa kikosi wanachukulia kua tukio hili ni la kukusudia linalenga kupunguza uwezo wa kisiraha wa kikosi hiki, na wameahidi kufanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hili. Tunapenda kufahamisha kua moja ya hazina za siraha za kikosi hiki iliripuka kabla ya siku chache katika kitongoji cha Wandi kilometa (20) kaskazini ya Karbala.

Ushahidi wa awali unaonyesha kua jana ilipita ndege isiyo kua na rubani juu ya eneo hilo, na adhuhuri ya leo imesikika sauti inayo ashiria kushambuliwa kwa hazina hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: