Kuomboleza kifo cha Imamu Aljawaad (a.s): Atabatu Abbasiyya tukufu yawekwa mapambo meusi na yaandaa ratiba maalumu ya kuomboleza msiba huu…

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) mwishoni mwa mwezi wa Dhulqa’ada huishi katika hali ya huzuni kubwa kufuatia msiba walio pata watu wa nyumba ya Mtume mwaka wa (220h), ambapo ni kumbukumbu ya kifo cha mwezi wa tisa miongoni mwa miezi ya Muhammadiyya (kizazi cha Mtume Muhammad) Imamu Aljawaad (a.s), Mu’utaswimu Abbasiy katika zama zake aliufanyia uislamu na waislamu dhambi kubwa, iliyo huzunisha moyo wa Mtume (s.a.w.w) na ukamliza bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na kuunyong’onyesha moyo wa Amirulmu-uminina (a.s), kwa kumuua Imamu miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) ambao Mwenyezi Mungu mtukufu ameufaradhishia umma huu kuwapenda.

Kufuatia kumbukumbu ya msiba huu Atabatu Abbasiyya tukufu ina ratiba endelevu ya kuomboleza misiba ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) pamoja na dhulma walizo fanyiwa, huzuni imetanda katika Ataba tukufu na imeandaliwa ratiba kamili ya kuomboleza msiba huu ambayo ina vipengele vingi, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira ya huzuni katika korido zote za malalo matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kufanya mihadhara ya kuomboleza ndani ya uwanja wa haram tukufu, na kufanya majlisi za kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala, pamoja na kujiandaa kupokea waombolezaji wanaokuja mmoja mmoja na wanaokuja kwa vikundi, na kufanya matembezi ya kwenda kumpa pole Imamu Hussein (a.s) katika malalo yake matukufu.

Kumbuka kua Imamu Aljawaad (a.s) alizaliwa katika mji wa Madina mwezi kumi Rajabu mwaka wa (195h), na alichukua madaraka ya uimamu tangu akiwa mdogo, alikua na miaka (7) au (8), muda wa Uimamu wake ulidumu kwa miaka (17) na alipewa majina ya sifa (laqabu) ya Aljawaad, Ataqiyyu, Alqaani’u, Azakiyyu na Baabu Almuraadu, alifariki mwishoni mwa mwezi wa Dhulqa’ada mwaka wa (220h) kwa kupewa sumu chini ya amri ya Mu’utaswimu Abbasiy, Jafari mtoto wa Ma-amuun aliwasiliana na dada yake Ummul Fadhil ambaye alikuwa mke wa Imamu Aljawaad (a.s), akamshawishi na kumuonyesha mbinu za kumuua (Abuu Jafari) mume wake (a.s) kwa kutumia sumu naye akakubali, akachukua sumu kali na akamuwekea mume wake katika chakula, Imamu alipo kula chakula hicho alihisi maumivu makali, kisha Ummul Fadhil alijuta kwa kitendo alicho fanya, akaanza kulia, Imamu akamuambia: (Wallahi utapatwa na ufakiri usio isha na balaa lisilo isha), alipata maradhi katika mwili wake, akatumia mali zote hadi zikaisha bila kupona, na Jafari mtoto wa Ma-amuun alidondoka ndani ya kisima kirefu akatolewa humo akiwa amekufa, na Imamu (a.s) aliungana na baba zake watakasifu (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu (Hakika sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake ndio marejeo yetu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: