Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya majlis za kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s)…

Maoni katika picha
Hakika kufanya majlis za kuomboleza watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ni miongoni mwa mambo yenye athari kubwa kiroho, humfanya mtu awe katika hali ya kukumbuka karama na utukufu wa maimamu wake wakati wote, na zinamsukuma kuwaiga na kufuata mwenendo wao, pia huongeza imani na kushikamana zaidi na itikadi yake na kunaongeza uwelewa na msimamo.

Miongoni mwa ratiba maalumu ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), msiba huu mchungu ulio umiza umma wa kiislamu kwa ujumla hususan watu wa nyumba ya Mtume (a.s) mwaka (220h), uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya siku mbili mfululizo umefanya majlis maalumu za kuomboleza kwa watumishi wake katika ukumbu wa utawala, imekua kawaida kufanya majlis za kuomboleza katika kumbukumbu za huzuni za watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Majlis zilikua na vipengele vingi, siku ya kwanza ilikua na mhadhara wa dini ulio tolewa na Sayyid Ahamad Mussawi na kumaliziwa na kaswida za kuomboleza, siku ya pili ilikua na muhadhara wa dini ulio tolewa na Sayyid Adnaan Mussawi na kumaliziwa na kaswida ya kuomboleza, masayyidi walio toa mihadhara wanatoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mihadhara yao wamezungumzia mambo muhimu na utukufu wa Imamu Aljawaad (a.s), wakawahimiza waumini na vijana umuhimu wa kupambika na tabia tukufu za Imamu huyu, na waifanye historia na mwenendo wake kuwa taa na bendera katika kujenga jamii, pia walizungumzia sehemu ya maisha ya Imamu (a.s) pamoja na matukio makubwa kihistoria aliyo kutana nayo, na msimamo gani alio kuwa nao katika kupambana na changamoto za kijamii na kisiasa, wakaelezea baadhi ya matukio katika historia ya Imamu Aljawaad (a.s).

Kuhusu kaswida za kuomboleza; zilibainisha namna Imamu Aljawaad alivyo fariki kwa sumu akiwa na kiu, na uhusiano wa kifo chake na cha babu yake bwana wa mashahidi (a.s) katika tukio la Twafu (Karbala).

Tunapenda kufahamisha kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya maombolezo na imewekwa mapambo meusi, na vitengo vyake vyote vimejiandaa kupokea waombolezaji wote na mawakibu za Husseiniyya katika mnasaba huu uumizao, pia kutakua na matembezi maalumu ya kuomboleza yatakayo fanywa na Ataba mbili tukufu Alasiri ya Juma Pili kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: