Mwishoni mwa mwezi wa Dhulqa’ada wa mwaka (220h) Mu’utaswimu bun Haruna Al-Abbasi alifanya dhambi ambayo tunakosa maneno ya kuielezea, na akili inashindwa kuamini, alimuua Hoja wa Mwenyezi Mungu katika ardhi Imamu Muhammad bun Ali Aljawaad (a.s).
Baada ya maudhi makubwa aliyopata Imamu wetu Aljawaad (a.s) katika uhai wake, ilimuijia faraja kama anavyo sema mwenyewe (a.s), baada ya miaka miwili na nusu ya kifo cha Ma-amuun alikua anasema (a.s): (Faraja baada ya Ma-amuun kwa muda wa miezi thelathini), ni dalili ya ukubwa wa mateso na mitihani aliyopata wakati wa uimamu wake kutoka kwa madhalimu hao, hadi akaona kifo ni faraja kwake (a.s).
Imamu (a.s) alikua anainua mikono juu na anasema: (Ewe Mola ikiwa faraja yangu ipo katika kifo kifanye kije haraka), kwa hiyo Imamu (a.s) alikua mwenye huzuni muda wote hadi alipo fariki kwa njama ya watu watatu, Mu’taswim, mtoto wa ndugu yake Jafari bun Ma-amuun na dada yake Ummul Fadhil mtoto wa Ma-amuun, aliye kua mmoja wa wake wa Imamu Aljawaad (a.s), ndiye aliye muwekea sumu Imamu (a.s) katika zabibu, Imamu alipata kiu kali kutokana na athari ya sumu hiyo, lakini pia (mke huyo) alimzuia kunywa maji, akamuombeleza babu yake bwana wa mashahidi (a.s) na akafa kwa sumu wakati anakiu, akiwa na umri wa miaka ishirini na tano.