Kwa maneno ya huzuni na majonzi makubwa sauti za vilio zasikika zikiita ,Waa Imamaahu waa Jawadaahu waa Madhlumaahu waa Masmumaahu huku macho yanatoka machozi na nyoyo zikiwa zimejaa huzuni kutokana na tukio la kuuawa kishahidi kwa Imamu wa tisa miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) katika ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuomboleza msiba huu, baada ya Adhuhuri ya leo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya matembezi ya kwenda kuomboleza kwa babu yake Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na kumbukumbu ya tukio hili chungu.
Matembezi yalianzia katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kujipanga katika vikundi na kusoma kaswida za kuomboleza, walianza kutembea wakielekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakiwa wamebeba jeneza la kuigiza la Imamu Madhlumu aliye uwawa kwa sumu (a.s) matembezi hayo yaliishia katika kuungana na washiriki wa Atabatu Husseiniyya tukufu na wakaimba kwa pamoja kaswida za kuomboleza zilizo kua na maneno ya kuamsha hisia za majonzi kutokana na tukio hili chungu lililo waumiza wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika siku kama ya leo ya mwisho wa mwezi wa Dhulda’ada mwaka wa (220h).
Makatibu wakuu wote wawili wa Atabatu Husseiniyya tukufu na Atabatu Abbasiyya wameshiriki katika matembezi haya pamoja na idadi kubwa ya viongozi na marais wa vitengo mbalimbali bila kuwasahau mazuwaru watukufu.
Tunapenda kufahamisha kua Atabatu Abbasiyya imesha andaa ratiba kamili ya maombolezo na imewekwa mapambo meusi pamoja na kutangaza maombolezo ya msiba huu, imejiandaa kikamilifu kupokea vikundi vya waombolezaji na mawakibu za Husseiniyya kufuatia tukio hili chungu.