Marhaba, Siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulhijja ambayo zilikutana bahari mbili na zikakaribiana nyota mbili…

Maoni katika picha
Siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulhijja mwaka wa pili hijiriyya; hitimisho la Manabii na Mitume Muhammad (s.a.w.w) alimuozesha mbora wa wanawake wa ulimwenguni bibi Fatuma Zaharaa kwa Amirulmu-uminina Ali bun Abu Twalib (a.s) na ikaitwa ndoa ya (Nuru mbili), tukio hili lina umuhimu mkubwa sana kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kwa sababu ni tukio la pekee na wote wawili ni watu watukufu, na Maimamu watakasifu ni matunda ya ndoa hii tukufu, tukio hili pia linaonyesha utukufu wa Imamu Ali (a.s) kwa Mtume (s.a.w.w).

Mwenyezi Mungu mtukufu alitaka familia ya Mtume (s.a.w.w) iendelee kupitia bibi Fatuma (a.s), matunda ya ndoa hii tukufu yalikua ni watoto wa kiume watatu na wa kike wawili ambao ni: Maimamu wawili watakasifu Hassan Almujtaba na bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), na watoto wa kike ni Aqilatu bani Haashim Zainabu Alkubra na Ummu Kulthum (a.s) walizaliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w) ndani ya muda wa miaka tisa, na mtoto wao wa mwisho ni Muhsin (a.s) aliye uwawa akiwa tumboni mwa mama yake baada ya siku chache tangu kufariki Mtume (s.a.w.w) kutokana na tukio la kumkandamiza bibi Fatuma baina ya ukuta na mlango lililo fanywa na wanafiki na madhalimu.

Baina ya ndoa ya mbinguni na ile ya ardhini kulikua na muda wa siku arubaini, aliye kua upande wa Ijaabu (tamko) la kuozesha ni Mwenyezi Mungu mtukufu na upande wa tamko la kukubali alikua ni Malaika Jibrilu, na khutuba ilisomwa na Malaika Rahiil na mashahidi walikua na Malaika wabeba Arshi na Malaika wengine elfu Sabini, na aliye husika na manukato ni Malaika Ridhwaan mtunzaji wa pepo, aliweka manukato ya Yakuti na Marjaani, na aliye husika na vazi la harusi ni Asmaa au Ummu Aiman na watoto wa ndoa hiyo ni Maimamu watakasifu (a.s).

Imepokewa na Sayyid Amiin katika kitabu chake cha Almajaalisu Saniyya maelezo ambayo kwa ufupi yanasema: Ali (a.s) alikwenda kwa Mtume (s.a.w.w) akiwa katika nyumba ya Ummu Salama, akamtolea salamu na akakaa mbele yake, Mtume (s.a.w.w) akamuuliza: Una shida? Akajibu (a.s): (Ndio: Nimekuja kumposa binti yako Fatuma (a.s), je! Utaniozesha)?.

Ummu Salma anasema: Nikaona uso wa Mtume (s.a.w.w) umejaa bashasha na furaha, akatabasamu mbele ya uso wa Ali (a.s) akasimama na kuingia kwa Fatuma (a.s), akamuambia: (Hakika Ali ameniambia jambo kuhusu wewe, na mimi nilimuomba Mola wangu akuozesho mtu bora, unaonaje)? Akanyamaza (a.s).

Mtume (s.a.w.w) akatoka huku anasema: (Mwenyezi Mungu mkubwa, kunyamaza kwake ni kukubali kwake). Mtume (s.a.w.w) akamuambia Anasi bun Maalik awaite maswahaba, ili awatangazie habari ya ndoa ya Fatuma na Ali (a.s), maswahaba walipo kusanyika Mtume (s.a.w.w) akawaambia: (Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameniamrisha nimuozeshe Fatuma mtoto wa Khadija kwa Ali bun Abu Twalib).

Kisha Mtume (s.a.w.w) akamuambia Ali kuwa Mwenyezi Mungu amemuamrisha amuozeshe Fatuma kwa gram mia nne za fedha.

Mapokeo: [Manaaqib Aali Abu Twalib (a.s), Bihaarul Anwaar, Majma’a Nuurain na Misbaahul Mujtahid].
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: