Kufuatia kutabaruku na kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili Ali na Fatuma (a.s): Kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu chashuhudia ongezeko kubwa la ufungishaji wa ndoa…

Maoni katika picha
Hakika siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulhijja ni siku tukufu mno, siku ambayo dunia ilinawirika na mbingu zikang’aa, kwa kukutana nuru mmbili na kufungwa ndoa takatifu na Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, katika mazingira matukufu mno yasiyo kua na mfano katika dunia, pope zilipambwa na mahurain walijiandaa kusherehekea harusi ya mbora wa wanawake na Ali mgawaji wa pepo na moto, ndoa hiyo tukufu ilisherehekewa mbinguni kabla ya wanadamu hawajaisherehekea hapa duniani.

Idara imeshuhudia ongezoko kubwa la ufungaji wa ndoa mpya, kwa ajili ya kutabaruku na ndoa ya Amirulmu-uminina na bibi Fatuma Zaharaa (a.s), huanza kupokea watu wanaokuja kuomba wafungishwe ndoa kuanzia asubuhi, wengi ambao wamefungishwa ndoa ni wale ambao waliahirisha kufunga ndoa zao kwa ajili ya kusubiri tarehe hizi tukufu, na wala sio watu wa Karbala peke yake, kuna watu wamekuja kutoka mikoa mingine.

Kumbuka kua ndoa zinafungishwa kwa kufuata sheria na masharti ya ndoa chini ya usimamizi wa mmoja wa Masayyid au Mashekhe wanaofanya kazi katika kitengo tajwa hapo juu pamoja na kuwaombea dua na kuwataka waishi maisha mema ya ndoa ili wamfurahishe Mtume wao na Ahlulbait watakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: