Kufuatia kazi ya uwekaji wa marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s): imeanza kazi ya awali ya uwekaji wa marumaru katika milango yake…

Maoni katika picha
Kufuatia kazi inayo endelea hivi sasa ya kuweka marumaru katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mafundi na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kuweka marumaru katika sehemu za milango ya zamani zinazo ungana na uwanja wa haram, kwa ajili ya kujiandaa kuweka marumaru katika uwanja huo, kwa kufuata vipimo maalumu vya eneo hilo na mwendelezo wa uwekaji wa marumaru.

Sehemu za upande wa nje wa milango zilijengwa wakati wa mradi wa upanuzi wa milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zikabaki sehemu za ndani za milango ya zamani zinazo ungana na uwanja wa haram tukufu, kazi ya ujenzi imeanza kwa kuondoa marumaru za zamani na kuandaa eneo kwa ajili ya kazi ya uwekaji wa marumaru chini ya vipimo maalumu na kwa namna ambayo haitawakwaza mazuwaru, utendaji wa kazi umeanzia katika mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) ambao upo upande wa nguzo ya mashariki, kaskazini ya uwanja mtukufu.

Kumbuka kua kazi ya hatua ya kwanza ya uwekaji wa marumaru katika uwanja wa haram tukufu ilihusisha sehemu za kuta za korido pamoja na sakafu zake zilizopo chini ya sehemu zilizo wekwa kashi karbalai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: