Kiongozi wa idara ya harakati za mahema ya Skaut, Ali Hussein Abduzaid ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hema hili la skaut lina malengo ya kutoa malezi ya kiroho na kuinua kiwango cha uzalendo na maarifa kwa washiriki pamoja na kunufaika na mazingira mazuri ya kiroho katika haram ya Amirulmu-uminina (a.s), na kukutana na Maraajii dini watukufu ikiwa kama sehemu ya kuwajenga kifikra kwa kukutana na Maraajii hao pamoja na viongozi mbalimbali wa hauza tukufu”.
Akaongeza kua: “Vile vile wanatembelea taasisi mbalimbali na vituo vya elimu kikiwemo kituo cha Imamu Mahdi (a.f) na baadhi za taasisi za kitamaduni, pamoja na kwenda katika maeneo ya kupumzika na kuwapa nafasi ya kubarizi vijana”.
Akabainisha kua: “Ratiba ya hema hizi imedumu kwa muda wa siku tatu na ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni:
- - Kumzuru Amirulmu-uminina (a.s) kwa pamoja na kutembelea maeneo ya Atabatu Alawiyya tukufu na baadhi ya vitengo vyake.
- - Kutembelea Maraajii dini watukufu na kupata nasaha zao tukufu.
- - Kutolewa mihadhara ya kidini, kiutamaduni na kifikra.
- - Kutembelea Masjid Kufa na maeneo yanayo fungamana na Masjid hiyo.
- - Kutembelea taasisi na vituo vya kielimu kikiwemo kituo cha Imamu Mahdi (a.s) na kituo cha fajru Aashuraa kilicho chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu.
- - Vipindi vya mapumziko.
- - Kufanya majlis maalumu za kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Kumbuka kua ratiba ya kujenga uwezo ya majira ya kiangazi awamu ya pili imeboreshwa, ni ratiba iliyo andaliwa kwa wanaskauti wa vikosi vitatu wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nane, kila kikosi kiliandaliwa ratiba inayo endana na umri wao, ratiba zimejaa nadwa na warsha zenye mihadhara mbalimbali zinazo toa elimu kwa nadhariya na vitendo katika sekta tofauti zinazo inua viwango vya elimu na vipaji vyao pamoja na kukomaza fikra zao.