Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla kuadhimisha kumbukumbu ya ndoa ya nuru mbili Ali na Fatuma (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa Baraka za Mwenyezi Mungu alizo wapa umma huu ni kuwaletea Mtume Muhammad pamoja na kizazi chake kitakatifu.. uwepo wao ni kheri nyingi.. katika siku kama hizi macho yalinawirika kwa kushuhudia ndoa ya nuru mbili.. nuru ya kijana wa bani Hashim ambaye Malaika Jibrilu alimsifu kwa kusema: “Hakina kijana ispokua Ali wala hakuna jambia ispokua Dhulfikaar..”, na nuru ya pande takatifu ambalo Mtume (s.a.w.w) alisema: “Fatuma ni pande litokanalo na mimi atakaye muudhi atakua ameniudhi”.

Katika kumbukumbu ya tukio hili tukufu –la kuowana nuru mbili- nuru ya Mwenyezi Mungu ni kubwa zaidi ndiyo iliyo pelekea kutokana na wao wawili zikapatikana nuru za Maimamu watakasifu (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya alasiri ya Juma Nne (2 Dhulhijja 1439h) sawa na (14 Agosti 2018m) imefanya hafla ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Ali Amuuriy pia wasomaji wa kaswida za Husseiniyya wakashiriki, ambao ni Mulla Ahmadi Alkinaani, Mulla Qahtwaani Albadiri na Mulla Hussein Zaghair Alkarbalai, walisoma mashairi mazuri sana kuhusu Imamu wetu Amirulmu-uminina Ali bun Abu Twalib (a.s) na bibi yetu mtakasifu Fatuma Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: